tenzi za rohoni
Tenzi za rohoni
Contents
45 Mtazame Huyo aliyeangikwa juu
50 Yesu nakupenda, U mali yangu
64 Ujaribiwapo, sifanye dhambi
80 Wamwendea Yesu kwa kusafiwa
91 Mapenzi yako yafanyike, Bwana
94 Siku ya mbingu kujawa na sifa
112 Nilikupa wewe maisha yangu
114 Bwana Mungu, nashangaa kabisa
136 Msifuni, Yesu ndiye mkombozi
138 Tukutendereza Yesu (Luganda)
141 Pana jito, lina maji mazuri
159 Ushirika mkuu, furaha yangu
160 Jioni moyo wangu wakutafuta
1 Mwokozi umeokoa
1.
Mwokozi umeokoa,
Nimekuwa
wako wewe.
Damu
imenisafisha;
Sifa
kwa mwana Kondoo.
Utukufu,
Aleluya!
Sifa
kwa Mwana Kondoo!
Damu
imenisafisha,
Utukufu
kwa Yesu!
2.
Nilijitahidi sana
Ila
sikupata raha;
Bali
kwa kumtegemea
Nilipata
Baraka.
3.
Daima namwegemea
Damu
ikifanya kazi,
Nikioga
kwa chemichemi
Itokayo
Mwokozi.
4.
Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi
kwako wewe:
Fahari
nashuhudia
Ya
wokovu wa bure.
5.
Nasimama kwake Yesu,
Ameponya
roho yangu;
Ameniondoa
dhambi,
Anifanye
mzima.
6.
Nilikuwa kifungoni,
Niliteswa
na dhambi,
Nilifungwa
minyororo
Yesu
akanifungua.
7.
Sifa, ameninunua!
Sifa,
nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana
huhifadhi!
Sifa
zake milele.
2 Twamsifu Mungu
1.
Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia
na kupaa juu.
Aleluya!
Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya!
Usifiwe, utubariki.
2.
Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia
Mwokozi wetu.
3. Twamsifu
Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa
dhambi akazifuta.
4.
Twamsifu Mungu wa neema yote,
Ametukomboa
akatuongoza.
5.
Tuamshe tena, tujazena pendo,
Na
moyoni uwashe moto wa Roho.
3 Hata ndimi elfu
1.
Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi
kweli
Bwana
Yesu kumsifu,
Kwa
zake fadhili.
2.
Yesu, jina liwezalo
Kufukuza
hofu;
Lanifurahisha
hilo,
Lanipa
wokovu.
3.
Jina hilo ni uzima;
Ni
afya amani;
Laleta
habari njema;
Twalipiwa
deni.
4.
Yesu huvunja mapingu
Ya
dhambi moyoni;
Msamaha,
tena nguvu,
Twapata
rohoni.
5. Kwa
sauti yake vile
Wafu
hufufuka
Wakafurahi
milele,
Pasipo
mashaka.
6. Ewe
Yesu wangu Bwana,
Uwezo
nipewe,
Kuhubiri
kote sana,
Wote
wakujue.
4 Jina la Yesu, salamu!
1.
Jina la Yesu, Salamu!
Lisujudieni,
Ninyi
Mbinguni, hukumu
Na
enzi mpeni.
2.
Enzi na apewe kwetu,
Watetea
dini;
Mkuzeni
Bwana wenu,
Na
enzi mpeni.
3.
Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi
msifuni;
Mmeponywa
kwa neema,
Na
enzi mpeni.
4.
Wenye dhambi kumbukeni
Ya
msalabani,
Kwa
furaha msifuni,
Na
enzi mpeni.
5.
Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote
msifuni,
Na
enzi mpeni.
6.
Sisi na wao pamoja
Tu
mumo sifani,
Milele
sifa ni moja,
Ni
“Enzi mpeni.”
5 Jina lake Yesu tamu
1.
Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza,
tena hamu
Hutuondolea.
2.
Roho iliyoumia
Kwalo
hutibika,
Chakula,
njaani pia;
Raha,
tukichoka.
3.
Jina hili ni msingi,
Ngao,
ngome, mwamba,
Kwa
hili napata wingi,
Kwangu
ni akiba.
4.
Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu,
Kuhani,
Mwanzo,
Mwisho, Njia, Haki,
Uzima
kifoni.
5. Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu
kweli,
Ila
sifa zangu hizi,
Bwana
zikubali.
6. Na
utakaponiita,
Kuja
kwako Bwana,
Huko
kwako sitaacha
Kukusifu
sana.
6 Baba, Mwana, Roho
1.
Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila
tukiamka tunakuabudu
Baba,
Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe
Utatu, tunakusifu.
2.
Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea
shukrani zao
Wanakusujudia
malaika nao:
Wewe u
mwanzo, nawe u mwisho.
3.
Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu
wako hatuoni kosa;
U
Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke
yako, mwenzio huna.
4. Baba,
Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba
vyote vyakusifu:
Baba,
Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe
Utatu, tunakusifu.
7 Ni tabibu wa karibu
1. Ni
tabibu wa karibu;
Tabibu
wa ajabu;
Na
rehema za daima;
Ni
dawa yake njema.
Imbeni,
malaika,
Sifa
za Yesu Bwana;
Pweke
limetukuka
Jina
lake Yesu.
2.
Hatufai kuwa hai,
Wala
hatutumai,
Ila
kweli yeye ndiye
Atupumzishaye.
3.
Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twendeni
na amani
Hata
kwake Mbinguni.
4.
Huliona tamu jina
La
Yesu Kristo Bwana,
Yuna sifa
mwenye kufa
Asishindwe
na kufa.
5.
Kila mume asimame,
Sifa
zake zivume;
Wanawake
na washike
Kusifu
jina lake.
6. Na
vijana wote tena,
Wapendao
sana
Waje
kwake wawe wake
8 Taji mvikeni
1.
Taji mvikeni,
Taji
nyingi tena,
Kondoo
mwake kitini,
Bwana
wa mabwana;
Name
tamsifu
Alikufa
kwangu,
Ni
mfalme mtukufu,
Mkuu
wa Mbingu.
2.
Taji mvikeni
Mwana
wa bikira;
Anazovaa
kichwani
Aliteka
nyara;
Shiloh
wa wanabii,
Mchunga
wa watu,
Shina
na tanzu vya Yese,
Wa
Bethirehemu.
3. Taji
mvikeni
Bwana
wa mapenzi;
Jeraha
zake ni shani
Ni
vito vya enzi,
Mbinguni
hakuna
Hata
malaika
Awezaye
kuziona
Pasipo
kushangaa.
9 Yesu kwetu ni rafiki
1.
Yesu kwetu ni rafiki,
Hwamiwa
haja pia;
Tukiomba
kwa Babaye
Maombi
asikia;
Lakini
twajikosesha,
Twajitweka
vibaya;
Kwamba
tulimwomba Mungu
Dua
angesikia.
2. Una
dhiki na maonjo?
Una
mashaka pia.
Haifai
kufa moyo,
Dua
atasikia
Hakuna
mwingine mwema
Wa
kutuhurumia;
Atujua
tu dhaifu;
Maombi
asikia.
3. Je,
hunayo hata nguvu,
Huwezi
kuendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa
pia,
Watu
wange kudharau,
Wapendao
dunia,
Hukwambata
mikononi,
Dua
atasikia.
10 Usinipite!
1.
Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru
wengine,
Usinipite.
Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru
wengine,
Usinipite.
2.
Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti
napiga pale,
Nisamehewe.
3.
Sina ya kutegemea,
Ila
Wewe tu;
Uso
wako uwe kwangu;
Nakuabudu.
4. U
Mfariji peke yako;
Sina
Mbinguni,
Wala
duniani pote,
Bwana
mwingine.
11 Nina haja nawe
1.
Nina haja nawe
Kila
saa;
Hawezi
mwingine
Kunifaa.
Yesu,
nakuhitaji
Vivyo
kila saa!
Niwezeshe,
Mwokozi,
Nakujia.
2.
Nina haja nawe;
Kaa
nami,
Na
maonjo haya,
Hayaumi.
3.
Nina haja nawe;
Kila
hali,
Maisha
ni bure,
Uli
mbali.
4.
Nina haja nawe,
Nifundishe
Na
ahadi zako
Zifikishe.
5.
Nina haja nawe,
Mweza
yote,
Ni
wako kabisa
Siku
zote.
12 Ewe Roho wa Mbinguni
1. Ewe
Roho wa Mbinguni
Uje
kwetu sasa.
Ufanye
makazi yako
Ndani
ya Kanisa.
2.
Ndiwe mwanga, umulike
Tupate
jikana;
Mengi
kwetu yapunguka,
Tujalize,
Bwana.
3.
Ndiwe Moto, teketeza
Taka
zetu zote:
Moyo
na iwe sadaka
Ya
Mwokozi, yote.
4.
Ndiwe Umande, na kwako
Tutaburudika,
Nchi
kavu itakuwa
Ni
yenye Baraka.
5.
Roho wa Mbinguni uwe
Nasi
hapa chini,
Mwili
uufananishe
Na
kichwa Mbinguni.
13 Tafuta daima utakatifu
1. Tafuta
daima utakatifu;
Fanya
urafiki na Wakristo tu;
Nena
siku zotena Bwana wako,
Baraka
uombe kwa kila jambo.
2.
Tafuta daima utakatifu;
Uwe
peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia
mwokozi wako,
Utabadilishwa
kama alivyo.
3.
Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi
wako aew Yesu tu;
Katika
furaha au huzuni
Dumu
kumfuata Yesu Mwokozi.
4.
Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze
Roho moyoni mwako;
Akikuongoza
katika haki,
Hufanywa
tayari kwa kazi yake.
14 Yesu kwa imani
1.
Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke
yako;
Nisikie
sasa,
Na
kunitakasa,
Ni
wako kabisa
Tangu
leo.
2.
Nipe nguvu pia
Za
kusaidia
Moyo
wangu;
Ulikufa
wewe,
Wokovu
nipewe
Nakupenda
wewe,
Bwana
wangu.
3.
Hapa nazunguka
Katika
mashaka,
Na
matata;
Palipo
na giza
Utaniongoza
Hivi
nitaweza
Kufuata.
4.
Takuwa mzima
Nivushe
salama
Mautini;
Sina
hofu kamwe
Ukiwapo
name
Nami
nikwandame
Siku
zote.
15 Cha kutumaini sina
1.
Chakutumaini sina
Ila
damu yake Bwana,
Sina
wema wa kutosha
Dhambi
zangu kuziosha;
Kwake
Yesu nasimama,
Ndiye
mwamba: ni salama
Ndiye
mwamba: ni salama.
2.
Njia yangu iwe ndefu
Yeye
hunipa wokovu;
Mawimbi
yakinipiga
Nguvu
zake ndiyo nanga.
3.
Damu yake na sadaka
Nategemea
daima,
Yote
chini yakiisha
Mwokozi
atanitosha.
4.
Nikiitwa hukumuni,
Rohoni
nina amani
Nikivikwa
haki yake
Sina
hofu mbele zake.
16 Kumtegemea Mwokozi
1.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu
tamu kabisa;
Kukubali
neno lake
Nina
raha moyoni.
Yesu,Yesu
namwamini,
Nimemwona
thabiti;
Yesu,Yesu,yu
thamani,
Ahadi
zake kweli.
2.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu
tamu kabisa,
Kuamini
damu yake
Nimeoshwa
kamili.
3.
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu
tamu kabisa,
Kwake
daima napata
Uzima
na amani.
4.
Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu,Mpendwa
na Rafiki
Uwe
nami dawamu.
17 Namwandama Bwana
1.
Namwndama Bwana kwa alilonena
Njia
yangu huning’azia;
Nikimridhisha
atanidumisha
Taamini
nitii pia.
Amini
utii, njia pweke ni hii
Ya
furaha kwa Yesu: amini ukatii.
2.
Giza sina kwangu wala hata wingu
Yeye
mara huviondoa
Woga,
wasiwasi, sononeko, basi;
Huamini
nitii pia.
3.
Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa
mapenzi hunilipia;
Baa,
dhara, dhiki, vivyo hubariki
Taamini
nitii pia.
4.
Mimi sitajua raha sawasawa
Ila
yote Yesu kumpa;
Napata
fadhili na radhi kamili,
Taamini
nitii pia.
5.
Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani
na njia-njia;
Agizo
natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini
nitii pia.
18 Akifa Yesu nikafa naye
1.
Akifa Yesu nikafa naye
Uzima
upya huishi naye;
Humtazama
mpaka nje:
Nyakati
zote ni wake yeye.
Nyakati
zote nimo pendoni,
Nyakati
zote ni uzimani,
Humtazama
hata atokee,
Nyakati
zote mimi ni wake.
2.
Vita sipigi visivyo haki,
Na
Bwana wangu hapiganiki;
Beramu
yake haitwaliki,
Napo
po pote hila sitaki.
3.
Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo
yote aihimili;
Ananituliza
Imanweli,
Nyakati
zote mimi husali.
4.
Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi
chozi, wala siguni;
Sikuti
afa, ila kitini
Daima
hunifikiri mimi.
5.
Kila unyonge huusikia;
Kila
ugonjwa kwake hupoa;
Yesu
ni mwenye kuniokoa
Nyakati
zote hunijalia.
19 Ndiyo dhamana, Yesu
wangu
1. Ndiyo
dhamana, Yesu wangu;
Hunipa
furaha za Mbingu;
Mrithi
wa wokovu wake
Nimezawa
kwa Roho yake.
Habari
njema, raha yangu
Yesu
ndiye Mwokozi wangu,
Habari
njema, raha yangu
Yesu
ndiye mwokozi wangu.
2.
Kumsalimu moyo wangu,
Mara
namwona raha yangu;
Aniletea
malaika,
Wananilinda,
taokoka.
3.
Sina Kinyume, nashukuru,
Mchana
kutwa huja kwangu;
Usiku
kucha kuna nuru;
Mwokozi
wangu; ndimi huru.
4.
Hali na mali anitwaa!
Mara
namwona anifaa,
Nami
nangoja kwa subira;
Akiniita,
nije mara.
20 Ninaye rafiki naye
1.
Ninaye Rafiki naye
Alinipenda
mbele;
Kwa
kamba za pendo zake
Nimefungwa
milele;
Aukaza
moyo wangu,
Uache
mageule,
Mimi
wake, yeye wangu;
Ndimi
naye milele.
2.
Ninaye rafiki ndiye
Aliyenifilia;
Alimwaga
damu yake
Kwa
watu wote pia;
Sina
kitu mimi tena,
Nikiwa
navyo tele;
Pia
vyote ni amana
Ndimi
wake milele.
3.
Ninaye rafiki naye
Uwezo
amepewa;
Atanilinda
mwenyewe,
Juu
tachukuliwa;
Nikitazama
Mbinguni,
Hupata
nguvu tele;
Sasa
natumika chini,
Kisha
juu milele.
4.
Ninaye rafiki naye,
Anao
moyo mwema;
Ni
mwalimu, kiongozi,
Mlinzi
wa daima;
Ni
nani wa kunitenga
Na
mapenzi ya mbele?
Kwake
nimetia nanga,
Ndimi
wake milele.
21 Roho yangu hima
1.
Roho yangu hima, na taa yako
Kaiwashe
vyema, hapa si pako;
Nguvu
zote pia za duniani
Hazitakudhuru
ukiamini.
Yesu
yuko mbele, Yesu yu nyuma,
Yesu
vivyo kando, walindwa vyema.
2.
Adui shetani, na nguvu zake,
Bwana
ameshinda, kwa kifo chake;
Wewe
nguvu huna, huna kabisa,
Ndiwe
mpungufu, mnyonge hasa.
3.
Toka na mapema, mbele ya wote,
Omba,
bisha sana, maisha yote;
Vita
vikaliko, macho ukae,
Jivike
silaha, nawe sishindwe.
4.
Bwana Yesu ndiye kwako mchunga,
Neno
lake Bwana ndilo upanga;
Mbingu
zitakwisha, na nchi pia,
Neno
lake Bwana laendelea.
22 Kale nilitembea
1.
Kale nilitembea
Nikilemewa
dhambi
Nilikosa
msaada,
kuniponya
mateso.
Usifiwe
Msalaba!
Lisifiwe
kaburi!
Linalozidi
yote,
Asifiwe
Mwokozi!
2.
Hata nilipofika,
Mahali
pa Msalaba,
Palinifaa
sana,
Sitasahau
kamwe.
3.
Hicho ndicho chanzo,
Cha
kufurahi kwangu.
Hapo
ndipo mzigo,
Uliponituliwa.
4.
Panapo msalaba,
Kinatolewa
cheti,
Cha
kuingia Mbinguni,
Kisicho
cha kanisa.
5.
Yule Bwana mjinga,
Likwenda
bila cheti,
Kitumai
kwingia,
Kama
walio nacho.
6.
Lipofika langoni,
Akaulizwa
cheti,
Cha
kumwonyesha Bwana,
Akakutwa
hanacho.
7.
Lituhuzunishalo,
Ni
ninyi msio nacho,
Kuwa
kama mjinga,
Kwa
siku ya arusi!
8.
Ubavuni mwa Yesu,
Mlitokea
damu,
Chemchemi
ya uzima,
Itakasayo
roho.
Damuni
mwa Mwokozi,
Utafutiwa
dhambi,
Toka
rohoni mwako.
23 Ni salama rohoni mwangu
1.
Nionapo amani kama shwari,
Ama
nionapo shida;
Kwa
mambo yote umenijulisha,
Ni
salama rohoni mwangu.
Salama
rohoni,
Ni
salama rohoni mwangu.
2.
Ingawa shetani atanitesa,
Nitajipa
moyo kwani
Kristo
ameona unyonge wangu,
Amekufa
kwa roho yangu.
3.
Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa
msalabani;
Wala
sichukui laana yake,
Ni
salama rohoni mwangu.
4. Ee
Bwana himiza siku ya kuja,
Panda
itakapolia;
Utakaposhuka
sitaogopa
Ni
salama rohoni mwangu.
24 Mwokozi moyoni mwangu
1. Tangu
siku hiyo aliponijia,
Akae
moyoni mwangu,
Sina
giza tena, ila mwanga pia
Kwa
Yesu mwokozi wangu.
Amani
moyoni mwangu,
kwa
Yesu, Mwokozi wangu;
Sina
shaka kamwe,
Kwa
sababu yeye,
Yu
nami moyoni mwangu.
2.
Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi
wangu.
Dhambi
zangu zote zimeondolewa,
Na
Yesu, Mwanawe Mungu.
3.
Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika
Mwokozi wangu.
Hofu
zangu na hamu zimeondoka,
kwa
kuwa ninaye Yesu.
4.
Siogopi tena, nikiitwa kufa,
Yu
nami daima, Yesu.
Mlango
wa Mbinguni ni yeye pia,
“Tapita
humo kwa damu.”
5.
Nitaketi na yeye huko milele,
Nisifu
Mwokozi wangu.
Nina
raha moyoni majira yote,
Kwa
Yesu, Mwanawe Mungu.
25 Nimekombolewa na Yesu
1.
Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa
bei ya mauti yake
Nimekuwa
mtoto wake.
Kombolewa!
Nakombolewa
na damu;
Kombolewa!
Mimi
mwana wake kweli.
2.
Kukombolewa nafurahi,
Kupita
lugha kutamka;
Kulionyesha
pendo lake,
Nimekuwa
mtoto wake.
3.
Nitamwona uzuri wake,
Mfalme
wangu wa ajabu;
Na
sasa najifurahisha,
Katika
neema yake.
4.
Najua taji imewekwa
Mbinguni
tayari kwangu;
Muda
kitambo atakuja,
Ili
alipo, niwepo.
26 Yesu unipendaye
1.
Yesu unipendaye
Kwako
nakimbilia,
Ni
wewe utoshaye,
Mwovu
akinijia;
Yafiche
ubavuni,
Mwako
maisha yangu;
Nifiikishe
mbinguni
Wokoe
moyo wangu.
2.
Ngome nyingine sina;
Nategemea
kwako.
Usinitupe
Bwana ,
Nipe
neema yako,
Ninakuamania
Mwenye
kuniwezesha;
Shari
wanikingia,
Vitani
wanitosha.
3.
Nakutaka Mpaji
Vyote
napata kwako;
Niwapo
muhitaji,
Utanijazi
vyako;
Nao
waangukao
Wanyonge
wape nguvu;
Poza
wauguao,
Uongoze
vipofu.
4.
Bwana umeniosha
Moyo
kwa damu yako;
Neema
ya kutosha
Yapatikana
kwako;
Kwako
Bwana naona
Kisima
cha uzima;
Mwangu
moyoni Bwana,
Bubujika
daima.
27 Mungu ni pendo
1.
Mungu ni pendo, apenda watu;
Mungu
ni pendo, anipenda
Sikilizeni
furaha yangu,
Mungu
ni pendo, anipenda.
2.
Nilipotea katika dhambi,
Nikawa
mtumwa wa shetani.
3.
Akaja Yesu kuniokoa,
Yeye
kanipa kuwa huru
4.
Sababu hii namtumikia,
Namsifu
yeye siku zote.
28 Anipenda ni kweli
1.
Anipenda ni kweli;
Mungu
anena hili;
Sisi
wake watoto;
kutulinda
si zito.
Yesu
anipenda,
Yesu
anipenda,
Kweli
anipenda,
Mungu
amesema.
2. Kwa
kupenda akafa
Niokoke
na kufa;
Atazidi
taka,
Sana
ataniweka.
3.
Anipenda kabisa;
Niuguapo
sasa
Anitunza
Mbinguni
Nniliyelala
chini.
4.
Kunipenda haachi,
Tu
sote hapa chini
Baada
ya mashaka
Kwake
tanipeleka.
29 Baba yetu aliye Mbinguni
1.
Baba yetu aliye Mbinguni
Amenifurahisha
yakini
Kuniambia
mwake chuoni
Ya
kuwa nami Yesu pendoni.
Anipenda
Mwokozi Yesu,
Anipenda,
anipenda;
Anipenda
Mwokozi Yesu,
Anipenda
mimi.
2.
Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye
yu vivyo, hupenda kweli,
Hunirejeza
kwake moyoni;
Kweli
yu nami Yesu pendoni.
3.
Anipenda! Nami nampenda;
Kwa
wokovu alionitenda;
Akanifia
Msalabani
Kwa
kuwa nami Yesu pendoni.
4.
Haya kujua yanipa raha;
Kumuamini
kuna furaha;
Humfukuza
mara shetani,
Kwona
yu nami Yesu Pendoni.
5.
Sifa ni nyingi asifiwazo,
Moja
ni sana katika hizo,
Wala
siachi, hata Mbinguni,
Kwimba,
“Yu nami Yesu pendoni”.
30 Nilikuwa kondoo aliyepotea
1.
Nilikuwa kondoo aliyepotea,
Sikupenda
zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa
mwana asiyesikia,
Sikupenda
baba yangu wala kutulia.
2. Na
mchunga mwema alinitafuta,
Baba
kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
Karibu
ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
Waliniona
mnyonge, waliniokoa.
3.
Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
Aliosha
taka zangu, dhambi nyingi sana;
Kwa
vidonda vyangu alitia dawa.
Ndiye
aliyenipata, na kwake nalindwa.
4.
Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa
nampenda Baba, na mchunga pia;
Kwanza
nilitanga na kukosa sana,
Hivi
nyumbani mwa Baba sipotei tena.
31 Msingi imara
1.
Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha
pigwa kwa neno hili;
Aongeze
lipi? Mnayo pia
Kwa
Yesu mliomkimbilia.
2. Wambiwapo
vuka maji ya giza,
Mito
ya mashaka taipunguza;
Takupa
nawe, nikuwezeshe,
Ipata
kufaa, isikutishe!
3.
Utakapopishwa ndani ya moto
Nnguvu
nitakupa, upate pato;
Huteketezwi,
ila taka zako,
Na
zitasalia dhahabu zako.
4.
Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni
kwisha mapenzi yangu;
Nazo
zitakapowenea, ndipo
Mabegani
mwangu niwatwekapo.
5. Na
mtu aliyenitegemea
Kamwe
kwa adui sitamtia;
Nguvu
za jehanam zijapotisha,
Mtu
wangu kamwe sitamuacha.
32 Yesu awakubali wakosa
1.
Yesu awakubali,
Wakosa,
wahalifu,
Wambieni
wa mbali
Habari
ya wokovu.
Tangazeni
kwa bidii,
“Akubali
wakosa!”
Liwe
neno dhahiri,
“Akubali
wakosa!”
2.
Awakubali Bwana
Neno
lake amini
Watu
kila aina
Waje
kwake tengoni.
3.
Mimi ni safi moyo
Na
mbele ya sharia,
Aliye
safi roho
Kwake
ilitimia.
4.
Akubali wakosa;
Nami
anikubali;
Alivyonitakasa
Mbinguni
niwasili.
33 Dhambi ikikulemea
1.
Dhambi ikikulemea,
Kwa
Bwana rehema;
Hivi
sasa tegemea
Neno
la salama.
Tegemea,
tegemea,
akwita
sasa.
Ni
Mwokozi, ni
Mwokozi;
amini sasa.
2.
Yesu amemwaga damu
Ya
nyingi baraka;
Nawe
sasa oga mumu
Zioshwamo
taka.
3. Ni
njia yeye hakika
Hwongoza
rahani;
Usikawe
kumshika,
Uwe
barakani.
4.
Karibu nawe wingie
Mwetu
safarini,
Twende
tukamwamkie,
Milele
Mbinguni.
34 Njoni! Wenye dhambi
1.
Njoni! Njoni! Wenye dhambi,
Njoni,
msikawie;
Yesu
awangojea ndiye awapendaye;
Ajuaye
awezaye
kuwaponya
ni Yeye.
2. Ewe
muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani,
kweli, na toba,
Neema
ya kutosha,
Jua
sana, kwake Bwana
Bure
utapata.
3.
Njoni, mliolemewa
Na
dhambi ya Adamu;
Mkingoja
kujiponya
Mtapotea
mumu;
Si wa
haki, ni wakosa
Waoshwao
kwa damu.
4.
Ikamtokea dhiki,
Mle
Gethisemani;
Kisha
alipoangikwa
Akalia
mtini;
”
Imekwisha”, alitosha
Dhabihu
ya thamani.
5.
Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea
huko;
Basi mtumai
yeye;
Kamwe
mwingine hako
Yesu
pweke, Yesu pweke,
Ndiye
Mwokozi wako.
6.
Wamsifu-sifu sana
Mbinguni
malaika;
Wachanganya
nyimbo zao
Na
waliookoka:
Aleluya
wataimba
Waliooshwa
taka.
35 Twende kwake
1.
Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa,
Sasa
twende kwake, kwake Yesu sasa!
2.
Akwokoe. akwokoe, Bwana Yesu sasa!
Sasa
akwokoe, Bwana Yesu, sasa!
3.
Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa,
Sasa
msadiki, Bwana Yesu sasa!
4.
Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa,
Sasa
anaweza, Bwana Yesu sasa!
5.
Anapenda, anapenda, Bwana Yesu, sasa,
Sasa
anapenda, Bwana Yesu sasa!
6.
Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa,
Sasa
njoo hima, kwake Yesu, sasa!
36 Anisikiaye aliye yote
1.
Anisikiaye, aliye yote;
Sasa
litangae, wajue wote,
Duniani
kote neno wapate,
Atakaye
na aje!
Ni
“Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani
hata bara, na litangae;
Ni
Baba Mpenzi alinganaye
Atakaye
na aje.
2.
Anijiliaye, Yesu asema,
Asikawe,
aje hima mapema;
Ndimi
njia, kweli, ndimi uzima;
Atakaye
na aje!
3.
Atakaye aje, ndivyo ahadi;
Atakaye
hiyo, haitarudi!
Atakaye
lake, ni la abadi!
Atakaye
na aje.
37 Waitwa, mwovu, na Bwana
1.
Waitwa, mwovu, na Bwana
Umwendee
hima sana,
Usafiwe
dhambi zako,
Humwoni
ni mwema kwako?
Unaitwa!
Itika tu!
Umwendee
Bwana Yesu!
Sifiche
makosa yako,
Uungame
dhambi zako!
Kristo
tu umuamini,
Ndiyo
njia ua Mbinguni.
2.
Alilipa damu yake
Ili
kukukweza kwake;
Alikufa
yeye Bwana,
Mimi
nawe tuwe wema.
3.
Ukifanywa kuwa mwema
Mwishoni
utasimama,
Utaingia
rahani
Na
wapenzi wa zamani.
4. Ni
mwanga tu, nchi ile;
Uovu
hauko kule,
Kwamba
wataka ufike
Sharti
huku uosheke.
38 Twende kwa Yesu
1.
Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia
atwonya tuijue
Imo
Chuoni; na Mwenyewe,
Hapa
asema, Njoo!
Na
furaha tutaiona,
Mioyo
ikitakata sana,
Kwako,
Mwokozi, kuonana,
Na
milele kukaa.
2.
”Wana na waje”, atwambia,
Furahini
mkisikia,
Ndiye
mfalme wetu pia,
Na
tumtii, Njoo.
3.
Wangojeani? Leo yupo;
Sikiza
sana asemapo;
Huruma
zake zikiwapo,
Ewe
kijana, Njoo.
39 Mwenye dhambi huna raha
1.
Mwenye dhambi huna raha,
Sikiza
nakusihi,
Utapata
msamaha
Kwake
Yesu Mwokozi!
Njoo
hima, njoo hima,
Naye
atafurahi.
2.
Yesu anakwita sana
Naye
yuko Mbinguni;
Hofu
ya kifo hapana
Kwake
ukiamini.
Njoo
hima, njoo hima,
Utapata
amani.
3.
Hatakwita siku zote;
Ni ya
sasa nafasi.
Lete
na uchafu wote,
Kukawa
haipasi.
Njoo
hima, njoo hima,
Ni
wokovu halisi.
4.
Uzima uko kwa Bwana
Twae
uzima hasa
Bure
unapatikana,
Wokovu
twae sasa!
Njoo
hima, njoo hima,
Twae
utakatifu.
40 Nasikia kuitwa
1.
Nasikia kwitwa
Na
sauti yako
Nikasafiwe
kwa damu
Ya
kwangikwa kwako.
Nimesogea
Mtini pako,
Unisafi
kwa damu ya kwangikwa kwako.
2. Ni
mnuonge kweli,
Umenipa
nguvu,
Ulivyonisafi
taka,
Ni
utimilivu.
3.
Yesu hunijuvya;
Mapenzi,
imani;
Tumai,
amani, radhi,
Hapa
na Mbinguni.
4. Huipa
imara,
Kazi
yake, ndani:
Huongezeka
neema,
Ashindwe
Shetani.
5.
Huishuhudia,
Myoyo
ya imani
Ya
kuzipata ahadi,
Wakimuamini.
6.
Napata wokovu,
Wema
na neema;
kwako
Bwana nina nguvu
Na
haki daima.
41 Yesu aliniita, “Njoo”
1.
Yesu aliniita, “njoo,
Raha
iko kwangu,
Kichwa
chako ukilaze
Kifuani
mwangu.”
Nilikwenda
kwake mara,
Sana
nilichoka;
Nikapata
kwake raha,
Na
furaha tena.
2.
Yesu aliniita, “njoo,
Kwangu
kuna maji,
Maji
ya uzima, bure,
Unywe
uwe hai, ”
Nilikwenda
kwake mara
Na
maji nikanywa:
Naishi
kwake, na kiu
Kamwe
sina tena.
3.
Yesu aliniita, “njoo,
Dunia
ni giza,
Ukinitazama
nuru
Takung’arizia.”
Nilikwenda
kwake mara
Yeye
jua langu,
Ni
kila wakati mwanga
Safarini
mwangu.
42 Kivulini mwa Yesu
1.
Kivulini mwa Yesu kuna Kituo:
Kituo
mbali na hamu, kituo kilicho tamu.
Kivulini
mwa Yesu kuna kituo;
kivulini
mwa Yesu kuna kituo;
Raha
tu, mle; amani tupu,
Furaha
tele; kivulini mwa Yesu
Raha
tu, mle; amani tupu,
Furaha
tele; kivulini mwa Yesu.
2.
Kivulini mwa Yesu nina amani
Iliyopita
fahamu, tena itakayodumu.
3.
Kivulini mwa Yesu, nina furaha;
Furaha
yenye fahari, ya kueneza habari.
43 Yesu akwita
1.
Yesu akwita, chanena Chuo:
Uje
leo, uje leo;
Kwani
kusita? Akwita, Njoo;
Unatanga
upeo.
Hwita
leo, hwita leo.
Yesu
akwita kwa upole akwita leo.
2.
Waliochoka, wapumzike,
Hwita
leo, hwita leo:
Wenye
mizigo, wakamtweke,
wapate
mapumuo.
3.
Anakungoja, uliye yote,
Uje
leo, uje leo;
Uliyekosa
usijifiche:
Woshwe,
uvikwe nguo.
4.
Yesu asihi wakawiao,
Waje
leo, waje leo.
Watafurahi
waaminio;
Usije
kwani? Njoo.
44 Kukawa na giza dunia yote
1.
Kukawa na giza dunia yote,
Ni
Mwanga wa ulimwengu,
Ikaisha
ulipokuja yote,
Ni
mwanga wa ulimwengu.
Jua,
Yesu hana mwenziwe!
Nalipofuka
kama wewe:
Nakuombea
umwone nawe,
Ni
mwanga wa ulimwengu.
2.
Hatuna giza tudumuo mwake,
Ni
mwanga wa ulimwengu;
Tumwandamiapo
nyayoni mwake
Ni
mwanga wa ulimwengu.
3.
Enyi wa gizani wenye kutanga!
Ni
mwanga wa ulimwengu,
Kaulekeeni,
mpate lenga;
Ni
mwanga wa ulimwengu.
4.
Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu
Ni
mwanga wa ulimwengu:
Ni
nuru za mbingu kondoo wa Mungu
Ni
mwanga wa ulimwengu.
45 Mtazame Huyo aliyeangikwa juu
1.
Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu
Hivi
sasa upate ishi.
Mwenye
– dhambi dhaifu, mtazame tu
Wala
usifanye tashwishi.
Tazama!
Tazama! Tazama uishi!
Mtazame
huyo aliyeangikwa juu
Hivi
sasa upate ishi.
2.
Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi,
Na
makosa yako maovu!
Kama
deni zetu zote hakulipa
Mbona
imemwagika damu?
3. Si
kutubu na sala ikomboayo,
Ila
damu ndiyo salama;
Na aliyeimwaga
aweza, sasa,
Dhambi
zako kukufutia.
4.
Usiwe na shaka, Mungu amesema,
Hakuna
alilolisaza;
Hapo
alipokuja alitimiza
Kazi
zote alizoanza.
5.
Basi twae uzima, kwa kufurahi
Upokee
kwa Bwana, sasa;
Ujijue
hakika kwake kuishi
Yesu
aishiye kabisa.
46 Twae wangu uzima
1.
Twae wangu uzima,
Sadaka
ya daima;
Twae
saa na siku,
Zikutukuze
huku.
2.
Twae mikono nayo
Ifanye
upendavyo,
Twae
yangu miguu
Kwa
wongozi wako tu.
3.
Twae sauti yangu,
Niimbe
kwa Mungu tu;
Itwae
na midomo,
Ijae
neno lako.
4.
Twae dhanabu pia,
Na
yote ya dunia;
Twae
yangu hekima,
Upendavyo
tumia.
5. Nia
itwae, Mungu,
Haitakuwa
yangu;
Twae
moyo; ni wako,
Uwe
makazi yako.
6.
Twae mapenzi yangu,
Sifa
za moyo wangu;
Twae
kabisa nafsi
Nniwe
wako halisi.
47 Ni wako wewe
1. Ni
wako wewe, nimekujua,
Na
umeniambia;
Lakini
Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.
Bwana
vuta, vuta, nije nisongee,
Sana,
kwako mtini.
Bwana
vuta, vuta, nije nisongee,
Pia
damu ya thamani.
2.
Niweke sasa nikatumike
Kwa
nguvu za neema;
Uyapendayo
nami nipende,
Nizidi
kukwandama.
3.
Nina furaha tele kila saa
Nizungumzavyo
kwako,
Nikuombapo
nami napata kujua nia yako.
4.
Mapenzi yako hayapimiki,
Ila
ng’ambo ya liko.
Anasa
pia sitazijua,
Bila
kufika kwako.
48 Naweka dhambi zangu
1.
Naweka dhambi zangu
Juu
yake Bwana
Kuziondoa,
kwangu
Hulemea
sana;
Na
uaili wangu
Ameuondoa;
Dawa
yangu ni damu,
Kwa
hiyo napoa.
2. Na
uhitaji wangu
Nitamjuvisha
Kwa
upungufu wangu
Yeye
anatosha;
Majonzi
yangu yote
Na
mizigo yangu,
Atachukua
vyote
Yesu
Bwana wangu.
3. Na
roho yangu nayo,
Imechoka
sana;
Namletea
hiyo
Ilindwe
na Bwana;
Ni
jema jina lake,
Nalo
lapendeza,
Imanweli
na kwake
tutalitukuza.
4.
Natamani daima
Niwe
kama Bwana,
Mpole,
tena mwema,
Wa
mapenzi sana;
Zaidi
natamani
Kwenda
kwake juu,
Nikaone
mbinguni
Enzi
yake kuu.
49 Nitwae hivi nilivyo
1.
Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga
damu yako,
Nawe
ulivyoniita,
Bwana
Yesu,naja,naja.
2.
Hivi nilivyo;si langu
Kujiosha
roho yangu;
Nisamehe
dhambi zangu,
Bwana
Yesu,naja,naja.
3.
Hivi nilivyo; sioni
Kamwe
furaha moyoni;
Daima
ni mashakani,
Bwana
Yesu,naja,naja.
4.
Hivi nilivyo kipofu,
maskini
na mpungufu;
Wewe u
mtimilifu;
Bwana
Yesu,naja,naja.
5.
Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu
kukawa,
Na
wewe hutanikataa,
Bwana
Yesu,naja,naja.
6.
Hivi nilivyo;mapenzi
Yamenipa
njia wazi;
Hali
na mali sisazi,
Bwana
Yesu,naja,naja.
50 Yesu nakupenda, U mali yangu
1.
Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa
za dhambi sitaki kwangu;
Na
Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa
nakupenda, kuzidi pia.
2.
Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa
vile ulivyonipenda mbele,
Uhai
wako ukanitolea
Sasa
nakupenda, kuzidi pia.
3.
Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe
tulio dhambini;
Taji
ya miiba uliyoivaa,
Sasa
nakupenda, kuzidi pia.
4.
Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana
nawe kamwe siachi;
Hari
za kifo zikinienea,
Sasa
nakupenda, kuzidi pia.
5.
Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo
huko Mbinguni,
Tasema
na taji nitakayovaa
Sasa
nakupenda, kuzidi pia.
51 Mungu twatoa shukrani
Mungu
twatoa shukrani,
Kwa
kutulinda usikuni,
Na
kutuangalia mchana,
Kutuongoza
kila mara.
52 Yote namtolea Yesu
1.
Yote namtolea Yesu
Nampa
moyo wote,
Nitampenda
siku zote,
Namwandama
kila saa.
Yote
kwa Yesu,
Yote
kwa Yesu,
Yote
kwako, Ee mwokozi,
Natoa
sasa.
2.
Yote namtolea Yesu,
Nainamia
pake;
Nimeacha
na anasa,
Kwako
Yesu nipokee,
3.
Yote namtolea Yesu,
Nifanye
niwe wako;
Nipe
Roho yako, Bwana,
Anilinde
daima,
4.
Yote namtolea Yesu,
Nami
naona sasa;
Furaha
ya ukombozi,
Nasifu
jina lake,
53 Wewe umechoka sana
1.
Wewe umechoka sana?
Wataka
raha?
Kwake
Yesu utapata furaha.
2.
Alama anazo yeye?
Sasa!
makovu ya mikono, na miguu,
Na
mbavu.
3.
Nacho kimivukwa taji
Kichwa
cha huba?
Alivikwa
taji kweli miiba.
4.
Huku nikimfuata nipate nini?
Maonjo
nje na ndani amani.
5.
Kwamba namwandama Bwana,
Mwisho
ni nini?
Ni
furaha na salama
Mbinguni.
54 Yesu nataka kutakaswa sana
1.
Yesu nataka kutakaswa sana,
Nataka
moyo uwe enzi yako.
Ukiangushe
kilichoinuka
Unioshe
sasa niwe mweupe.
Mweupe
tu, ndiyo mweupe,
Ukiniosha
nitakuwa safi.
2. Bwaba
Yesu, unitazame sasa,
Unifanye
niwe dhabihu hai;
Najitoa
kwako, na moyo wote;
Unioshe
sasa niwe mweupe.
3.
Bwana kwa hiyo nakuomba sana,
Nakungojea
miguuni pako,
Naomba
unioshe damuni tu,
Unioshe
sasa niwe mweupe.
4.
Bwana nidumu kukungojea,
Niumbie
moyo safi, Ee Mungu,
Wanaokujia
hutupi kamwe,
Unioshe
sasa niwe mweupe.
55 Nipe moyo wenye sifa
1.
Nipe moyo wenye sifa
Sio wa
utumwa;
Moyo
ulionyunyizwa
Damu
ya thamani.
2.
Moyo msikizi, moyo
Wa
kunyenyekea,
Moyo
utawaliwao
Na
Mwokozi pia.
3.
Mwenye kutubu, mnyonge,
Sadiki,
amini;
Kamwe,
kamwe asitengwe
Akaaye
ndani.
4.
Mpya, mwema na mawazo
Mwingi
wa mapenzi
Nawe
uwe kielelezo
Moyo
wa Mwokozi.
5. Ni
uule moyo wako;
Moyo
wa huruma
Yesu,
natamani kwako
Kukujua
vyema.
6. Na
ya midomo matunda
Yako,
nipe nami;
Amani
isiyokoma
Iwe
yangu mimi.
7.
Nitie yako tabia,
Inishukie
juu;
Jina
lako nipe pia,
Ndilo
la upendo.
8. Ni
wa baba utukufu;
Mwana
atukuke;
Na
roho Mtakatifu
U
utatu pweke.
56 Ni sikukuu siku ile
1. Ni
siku kuu siku ile
Ya
kumkiri Mwokozi!
Moyo
umejaa tele,
Kunyamaza
hauwezi.
Siku
kuu! Siku kuu!
Ya
kuoshwa dambi zangu kuu!
Hukesha
na kuomba tu,
Ananiongoza
miguu.
Siku
kuu! siku kuu!
Ya
kuoshwa dhambi zangu kuu.
2.
Tumekwisha kupatana
Mimi
wake, yeye wangu,
Na
sasa nitamwandama,
Nikiri
neno la Mungu.
3.
Moyo tulia kwa Bwana
Kiini
cha raha yako,
Huna
njia mbili tena;
Yesu
ndiye njia yako.
4.
Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka
daima,
Hata
ije siku ile,
Ya
kwonana kwa salama
57 Naendea msalaba
1.
Naendea Msalaba,
Ni
mnyonge na mpofu,
Yapitayo
naacha,
Nipone
Msalabani.
Nakutumaini
tu,
Ewe
Mwana wa Mungu;
Nainamia
kwako;
Niponye,
mponya wangu.
2.
Nakulilia sana:
Nalemewa
na dhambi;
Pole
Yesu asema;
“Nitazifuta
zote”.
3.
Natoa vyote kwako,
Nafasi
nazo nguvu,
Roho
yangu na mwili,
Viwe
vyako milele.
4. Kwa
damu yake sasa,
Nimegeuka
roho,
Nikaziacha
tama
Nimfuate
Yesu tu.
5.
Yesu yuaja tena!
Nimepevuka
kwake,
Kila
chembe kamili;
Msifuni
yeye mponya!
58 Mwamba mwenye imara
1.
Mwamba wenye imara
Kwako
nitajificha!
Maji
hayo na damu
Yaliyotoka
humu,
Hunisafi
na dhambi,
Hunifanya
mshindi.
2. Kwa
kazi zote pia ,
Sitimizi
sharia.
Nijapofanya
bidii,
Nikilia
nakudhii,
Hayaishi
makosa;
Ndiwe
wa kuokoa.
3.
Sina cha mkononi,
Naja
Msalabani;
Nili
tupu, nivike;
Ni
mnyonge, nishike;
Nili
mchafu naja,
Nioshe
nisijafa.
4.
Nikungojapo chini,
Nakwenda
kaburini;
Nipaapo
Mbinguni,
Na
kukwona enzini:
Roho
yangu na iwe
Rahani
mwako wewe.
59 Peleleza ndani yangu
1.
Peleleza ndani yangu,
Iwe
safi nia,
Kwangu
kama kwako Mungu,
Idhihiri
pia.
2.
Peleleza moyo wangu
Uunifunulie,
Yaliyomo
ndani yangu
Nami
niyajue.
3.
Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga
giza;
Nijue
ambavyo dhambi
Ni la
kuchukiza.
4.
Peleleza na mawazo
Ni
mbegu za mambo,
Asili
ya machukizo,
Maumbuo
– umbo.
5.
Zidi kuyapeleleza
Katikati
yangu
Hata
wishe nifundisha
Udhaifu
wangu.
6.
Hapo nikikwinamia
Mbele
zako, Mungu,
Hakika
nitakujua
U
mpenzi wangu.
60 Waponyeni watu
1.
Waponyeni watu wamo kifoni,
Watoeni
walio shimoni;
Na
aangukaye mumzuie;
Ya
Bwana Yesu wahubirini.
Walio
kifoni waokoeni,
Mwokozi
yuko, wahubirini.
2.
Wajapokawia anangojea,
Awasubiri
waje tobani;
Msiwadharau,
muwaonyeni;
Huwasamehe;
wakiamini.
3.
Myoyoni mwa ndani, yule shetani
Ameyaseta
mawazo yao;
Lakini
kwa Bwana huwa mazima,
Tukiwavuta
kwa pole hao.
4.
Kawaokoeni, wale njiani,
Mutimize
mapenzi ya Bwana;
Na kwa
nguvu zake warudi kwake,
Kwa
subira waonyeni sana.
61 Tumesikia mbiu
1.
Tumesikia mbiu:
Yesu
lo! aponya,
Utangazeni
kote,
Yesu,
lo! aponya.
Tiini
amri hiyo;
Nchini
na baharini,
Enezeni
mbiu hii;
Yesu ,
lo! aponya.
2.
Imbeni na vitani;
Yesu,
lo! aponya;
Kwa
nguvu ya kombozi,
Yesu,
lo! aponya.
Imbeni
wenye shida,
Unapoumwa
moyo.
Na
karibuni imba;
Yesu,
lo! aponya.
3.
Mawimbini uenee;
Yesu,
lo! Aponya;
Wenye
dhambi jueni;
Yesu,
lo! Aponya.
Visiwa
na viimbe,
Vilindi
itikeni,
Na
nchi shangilieni;
Yesu,
lo! Aponya.
4.
Upepo utangaze;
Yesu,
lo! Aponya;
Mataifa
yashangaaa;
Yesu
lo! Aponya.
Milimani,
bondeni,
Sauti
isikike
Ya
wimbo wa ushindi;
Yesu,
lo! Aponya.
62 Bwana wa mabwana
1.
Bwana wa mabwana,
Mwenye
nguvu sana
Twakusihi:
Neno
la milele
Na
liende mbele,
Waongoke
tele
Kwa
Mwokozi.
2.
Tunaowaona
Wanavyopatana,
Kulipinga,
Hawataliweza
Neno,
kulitweza:
Huwaje!
Kucheza:
Na
upanga?
3.
Heri wajitunze
Ili
wapatane,
Na
Mwokozi;
Watafute
sana,
Wapate
kuona,
Yesu
kuwa Bwana,
Mkombozi.
4.
Mungu awaita
Wasije
kukuta
Pigo
lake;
Hakuona
vyema
Wakose
uzima,
Awape
rehema,
Waokoke.
5.
Mwenye utukufu
Tunamshukuru
Yeye
pweke!
Nasifiwe
sana,
Baba,
naye Mwana,
Na wa
tatu tena
Roho
yake.
63 Ndugu wa kirohoni
1.
Ndugu wa kirohoni
Mliokombolewa,
Tafakarini
sana
Yatupasayo.
Wapenzi
wake Yesu
Tuliokombolewa
Tujitoe
kabisa
Wengi
waponywe.
2.
Siku itatimia
Tutakapoulizwa
Wale
wa nyumba zetu
Na
majirani
3.
Tujitoeni, ndugu,
Tukahubiri
Injili.
Atutumie
Roho
kuponya
wengi.
4.
Wasiokombolewa
Ni
wengi vijijini,
Wataokolewaje
Tukiogopa?
5.
Bwana alijitoa
Akapotewa
mengi,
Ili
atuokoe,
Tusiwe
waoga.
6.
Aliyetununua,
Kwa
kuimwaga damu,
Angalieni
sana
Msimwepuke.
64 Ujaribiwapo, sifanye dhambi
1.
Ujaribiwapo, sifanye dhambi,
Bali
uzishinde, kwa Yesu kutii.
Fuliza
kiume ushinde tamaa;
Yesu
ni Mwokozi, hukuokoa.
Umwombapo
yu papo
Akuongeze
nguvu,
Atakusaidia;
Yesu
atakufaa.
2.
Wepushe waovu, matusi dharau;
Heshima
la Mungu, kamwe sisahau;
Fanya
uhodari, uwe mpole,
Atakuokoa
hata milele.
3.
Avumiliaye hupewa taji;
Tujaposumbuka
tu washindaji,
Na
mwokozi wetu hutuwezesha
Tusiwe
kushindwa kama twakesha.
65 Safari
1.
Katika safari yetu
Kwenda
Mbinguni
Tusiishe
siku zetu
Usingizini.
Ng’oani!
Tujifungeni,
Twende
zetu juu!
Kristo
ndiye kiongozi;
Tusihofu
tu.
2.
Atwekwe badala yetu,
Mwenyewe
Bwana;
Yesu
kiongozi wetu
Atapokea.
3.
Kisimani, maji tele,
Maji
mazima!
Maji
hayo,
Ya milele
Yana
neema.
4.
Njiani miiba mingi,
Yatuumiza;
Hofu
na hatari nyingi,
Sana
zakaza.
5.
Kweli, njia ya Mbinguni
Ni ya
mashaka;
Tuwe
na Yesu njiani,
Mara
hufika.
66 Po pote mashamba yajaa
1. Po
pote mashamba yajaa,
Tele
nafaka pevu,
Po
pote yang’aa meupe
Bondeni
na nyandani.
Mwenye
mavuno, wasihi
Upeleke
wavuni,
Wakusanye
mazao,
Hata
kazi iishe.
2.
Wapeleke uchaoni,
Waende
na jotoni,
Mpaka
jua lishukapo
Wakusanye
ko kote.
3.
Watenda kazi wa Bwana,
Mlete
sasa mazao,
Na
jioni ingieni
Kwake
na furaha kuu.
67 Bwana uliyewaita
1.
Bwana uliyewaita
Watakatifu
wako,
Wawe
mitume, wachunga,
Walishe
kundi lako;
wanyonge
na wenye hofu
Wakawa
mashujaa,
Na
wapole wa kunena
Wasiwe
kunyamaa.
2.
Hata leo wawataka
Watakatifu
wako,
Nawe
wauliza tena
Ni
nani aliyeko
Atakaye
nimtume
Afundishe
vijana?
“Ni
tayari, Bwana wangu,
Nitume
mimi Bwana.”
3.
Nitume na mimi, Bwana
Kama
ulivyotumwa,
Habari
ya msamaha
Na
dhambi kutubiwa,
Niwahubiri
wakosa,
Na
waliopotea,
Wokovu
u wake Bwana,
Aliyewafilia.
4.
Astahiliye hapana
Kutamka
habari,
Lakini
wewe waweza
Kutufanya
tayari.
Neno
lako tulijue,
Tupe
na roho yako,
Hayatakuwa
ya bure,
Haya
maneno yako.
68 Mungu msaada wetu
1.
Mungu msaada wetu
Tangu
myaka yote,
Ndiwe
tumaini letu
La
zamani zote.
2. Kivuli
cha kiti chako
Ndiyo
ngome yetu.
Watosha
mkono wako
Ni
ulinzi wetu.
3.
Kwanza havijakuwako
Nchi
na milima,
Ndiwe
Mungu; chini yako
Twakaa
salama.
4. Na
myaka elfu ni kama
Siku
moja kwako;
Utanilinda
daima
Tu
wenyeji wako.
5.
Binadamu huondoka,
Mwisho
hana kitu;
Kama
ndoto hutoweka
Ndivyo
hali yetu.
6. Ila
wewe Mungu wetu
Ndiwe
wa kudumu;
Ndiwe
bora, ngome yetu
Twakaa
dawamu.
69 Twendeni askari
1.
Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu
yuko mbele, tumwandame juu.
Ametangulia
Bwana vitani,
Twende
mbele kwani ndiye amini.
Twende
askari watu wa Mungu;
Yesu
yuko Mbele, tumwandame juu.
2.
Jeshi la Shetani, likisikia
Jina
la Mwokozi, litakimbia,
Kelele
za shangwe zivume nchi;
Ndugu
inueni zenu sauti.
3.
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
Sisi
na mababa tu moja fungu.
Hatutengwi
nao, moja imani,
Tumaini
moja, na moja dini.
4.
Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni
myoyo, nanyi sifuni;
Heshima
na sifa ni ya Mfalme,
Juu
hata chini, sana zivume.
70 Yesu atuchunga
1.
Yesu atuchunga,
Mchunga
wetu,
Naye
atufuta
Machozi
yetu;
Mkononi
mwake
Hatuna
hofu,
Daima
twapata
Kwake
wokovu.
2.
Yesu atuchunga
Tumemjua,
Na
sauti yake
Twaitambua;
Naye
akituonya
Ni kwa
upole,
Tu
kondoo zake
Hata
milele.
3.
Yesu atuchunga;
Aliwafia
Kondoo
wakubwa
Na
wana pia;
Kwamba
awajua,
Kondoo
zake,
Hutiwa
alama
Ya
damu yake.
4.
Yesu atuchunga;
Mikono
yake
Imewaambata
Kondoo
zake;
Hapati
wadhuru
Adui
yule,
Yesu
awalinda.
71 Mteteeni Yesu
1.
Mteteeni Yesu,
Mlio
askari;
Inueni
beramu,
Mukae
tayari,
Kwenda
nae vitani,
Sisi
hatuchoki
Hata
washindwe pia
Yeye
amiliki.
2.
Mteteeni Yesu,
Vita
ni vikali;
Leo
siku ya Bwana,
Atashinda
kweli,
Waume
twende naye,
Adui
ni wengi,
Lakini
kwake Bwana
Tuna
nguvu nyingi.
3.
Mteteeni Yesu,
Wenye
ushujaa;
Nguvu
zenu za mwili
Hazitatufaa;
Silaha
ya injili
Vaeni
daima,
Kesheni
mkiomba,
Sirudini
nyuma.
4.
Mteteeni Yesu,
Vita
ni vikali,
Wengi
wamdharau,
Hawamkubali,
Ila
atamiliki
Tusitie
shaka,
Kuwa
naye vitani
Twashinda
hakika.
72 Twendeni! Haraka!
1.
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
Liwe
mwanga kwa nchi zilizo giza.
Bwana
alisema nendeni po pote
Kawafundisheni
mataifa yote.
Pelekeni
Injili kwa jina la Yesu.
Upesi!
Twendeni haraka!
2.
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La
upendo wa Mungu kwa watu wote;
Aliyeupenda
sana ulimwengu
Akamtoa
Yesu Mwana wake pekee
Kaleta
wokovu, tumtangazeni.
Upesi!
Twendeni haraka!
3.
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno
La
uzima kwa watu waliokufa.
Mateka
ya Shetani litafungua
Litaponyesha
na kuwapa amani.
Twendeni
upesi, tukawaokoe.
Upesi!
Twendeni haraka!
73 Yesu zamani Bethilehemu
1.
Yesu zama Bethilehemu,
Aliyezaliwa
kwa aibu,
Ndiye
mwakozi wa ulimwengu,
Akaja
kwa mimi.
Akaja
kwa mimi; akaja kwa mimi;
Ndiye
mwaokozi wa ulimwengu,
Akaja
kwa mimi.
2.
Yesu akafa msalabani,
Kuniponya
akalipa deni,
Ni la
ajabu ya jinsi gani
Kunifia
mimi!
Kunifia
mimi! Kunifia mimi!
Ni la
ajabu ya jinsi gani
Kunifia
mimi.
3. Ni
yeye huyo tangu asili;
Na
nilipotanga-tanga mbali
Alikuja
kwa upole, kweli
Kuniita
mimi.
Kuniita
mimi; Kuniita mimi;
Alikuja
kwa upole, kweli
Kuniita
mimi
4.
Yesu kristo atarudi tena,
Hilo
lanifurahisha sana.
Yeye
Bwana akionekana
Kunijia
mimi.
Kunijia
mimi, kunijia mimi,
Yeye
Bwana akionekana
Kunijia
mimi
74 Wachunga walipolinda
1.
Wachunga walipolinda
Kucha nyama
zao,
Malaika
mtukufu
Alishuka
kwao.
2.
Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
“Nawaletea
habari
Ya
kuwapendeza.”
3.
”Mji ule wa Daudi
Leo
amezawa
Mwokozi
ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa”.
4.
”Huyo mwana wa Mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa
kihorini
Malazi
hapana.”
5.
Alipokwisha yanena
Malaika
hao
Waliimba
wimbo huu
Usio
na mwisho:
6.
”Enzi ni yake Munju juu,
Na
nchi salama,
Kwa
watu nao radhi kuu,
Sasa
na daima.”
75 Waimba, sikizeni
1.
Waimba, sikizeni,
Malaika
Mbinguni;
Wimbo
wa tamu sana
Wa
pendo zake Bwana,
“Duniani
salama,
Kwa
wakosa rehema.”
Sisi
sote na twimbe
Nao
wale wajumbe;
Waimba,
sikizeni,
Malaika
mbinguni.
2.
Ndiye Bwana wa Mbingu,
Tangu
milele Mungu,
Amezaliwa
mwili,
Mwana
wa mwanamwali;
Ametoka
enzini
Kuja
ulimwenguni
Mwokozi
atufie,
Ili
tusipotee.
Waimba,
sikizeni,
Malaika
Mbinguni.
3.
Mtukufu wa amani
Ametoka
Mbinguni,
Jua la
haki, ndiye
Atumulikiaye;
Amejivua
enzi,
Alivyo
na mapenzi,
Ataka
kutuponya,
Kutuzalisha
upya,
Waimba
sikizeni,
Malaika
Mbinguni.
4.
Njoo upesi, Bwana,
Twakutamani
sana;
Kaa
nasi, mwokozi
Vita
hatuviwezi;
Vunja
kichwa cha nyoka,
Sura
zako andika,
Tufanane
na wewe,
Kwetu
sifa upewe,
Waimba,
sikizeni,
Malaika
Mbinguni.
…
76 Njoni, enyi wa imani
1.
Njoni na furaha, enyi wa imani,
Njoni
Bethilehemu upesi !
Amezaliwa
jumbe wa Mbinguni;
Njoni
tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni
tumuabudu Mwokozi.
2.
Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga,
Amekuwa
radhi kuzaliwa;
Mungu
wa kweli, wala si kiumbe;
Njoni
tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni
tumuabudu Mwokozi.
3.
Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu,
Mbingu
zote na zijae sifa;
Sifuni
Mungu aliye Mbinguni;
Njoni
tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni
tumuabudu Mwokozi.
4. Ewe
Bwana mwema, twakubarikia,
Yesu,
utukufu uwe wako;
Neno
la Baba limekuwa mwili;
Njoni
tumuabudu, njonu tumuabudu,
Njoni
tumuabudu Mwokozi.
77 Msalabani pa Mwokozi
1.
Msalabani pa mwokozi,
Hapo
niliomba upozi,
Akaniokoa
mpenzi,
Mwana
wa Mungu.
Mwana
wa Mungu, Mwokozi wangu,
Akaniokoa
mpenzi, Mwana wa Mungu.
2.
Chini ya mti msumbufu,
Niliomba
utakatifu,
Alinikomboa
kwa damu,
Mwana
wa Mungu.
Mwana
wa Mungu, Mwokozi wangu,
Alinikomboa
kwa damu, Mwana wa Mungu.
3.
Aliniokoa dhambini,
Ikawa
kunikaa ndani,
Aliponifia
mtini,
Mwana
wa Mungu.
Mwana
wa Mungu, Mwokozi wangu,
Aliponifia
Mtini, Mwana wa Mungu.
4.
Damu ya Yesu ya thamani,
Huniokoa
makosani,
Huniendesha
wokovuni,
Mwana
wa Mungu.
Mwana
wa Mungu, Mwokozi wangu,
Huniendesha
wokovuni, Mwana wa Mungu.
5.
Hicho kijito cha gharama,
Leo
jivike kwa kuzama,
Kwake
uuone uzima,
Mwana
wa Mungu.
Mwana
wa Mungu, Mwokozi wangu,
Kwake
uu…
78 Sioshwi dhambi zangu
1.
Sioshwi dhambi zangu,
Bila
damu yake Yesu.
Hapendezewi
Mungu,
Bila
damu yake Yesu.
Hakuna
kabisa
Dawa
ya makosa
Ya
kututakasa,
Ila
damu yake Yesu.
2. La
kunisafi sina
Ila
damu yake Yesu.
Wala
udhuru tena,
Ila
damu yake Yesu.
3.
Sipati pataniswa,
Bila
damu yake Yesu.
Hukumu
yanitisha,
Bila
damu yake Yesu.
4.
Sipati tumaini,
Bila
damu yake Yesu.
Wema
wala amani,
Bila
damu yake Yesu.
5.
Yashinda ulimwengu,
Hiyo
damu yake Yesu.
Na
kutufikisha juu,
Hiyo
damu yake Yesu.
6.
Twaimba: Utukufu
Una
damu yake Yesu.
Milele
twaisifu,
Hiyo
damu yake Yesu.
79 Msalaba wa aibu
1.
Msalaba wa aibu,
Ulinipa
amani;
Uliniondoa
kifungoni,
Nilimotesekea.
2. Ee,
Mwokozi wangu, Yesu
Nitamwendea
nani?
Najiweka
msalabani,
Nikaoshwe
damuni.
3.
Nakupenda Bwana Yesu,
Kwa
kunipenda kwako,
Napendezwa
nikutumikie
Maisha
yangu yote.
4.
Usifiwe Bwana Yesu,
Kwa
ulivyonifia,
Aleluya,
nakushukuru,
Uliyenikomboa.
5.
Msalaba ulishinda
Nguvu
zake adui,
Ili
mimi nikombolewe,
Niwe
mwana wa Mungu.
80 Wamwendea Yesu kwa kusafiwa
1.
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na
kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je
neema yake umemwagiwa,
Tumeoshwa
kwa damu ya kondoo?
Kuoshwa,
kwa damu,
Itutakasayo
ya kondoo;
Ziwe
safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa
kwa damu ya kondoo?
2.
Wamwandama daima mkombozi
Na
kuoshwa na damu ya kondoo?
Yako
kwa msulubiwa makazi,
Umeoshwa
kwa damu ya kondoo?
3.
Atakapokuja Bwana –arusi
Uwe
safi kwa damu ya kondoo!
Yafae
kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe
kwa damu ya kondoo.
4.
Yatupwe yaliyo na takataka,
Na
uoshwe kwa damu ya kondoo.
Huoni
kijito chatiririka
Na
uoshwe kwa damu ya kondoo?
81 Chini ya msalaba
1.
Chini ya msalaba
Nataka
simama;
Ndio
mwamba safarini,
Wa
kivuli chema;
Ni kweli
kwa roho yangu
Ni tuo
kamili,
Tatua
mzigo wangu
Wakati
wa hari.
2.
Hapa ni pema sana,
Ni
ngome kamili;
Hapa
yameonekana,
Mapenzi
ya kweli;
Kama
alivyoonyeshwa
Yakobo
zamani,
Msalaba
umekuwa
Ngazi
ya Mbinguni.
3. Na
Yesu msalabani
Walimkemea,
Alikufa
niokoke
Niliyepotea;
Naona
ajabu sana
Ya
mambo mawili
Jinsi
alivyonipenda,
Nisiyestahili.
4.
Atakayeonana,
Na
Yesu Mbinguni,
Njia
yake aanzapo
Ni
msalabani;
Wokovu
upo hapa tu,
Mwingine
hapana,
Kisha
kuna furaha kuu
Pamoja
na Bwana.
82 Sioni haya kwa Bwana
1.
Sioni haya kwa Bwana
Kwake
nitang’ara!
Mti
wake sitakana,
Ni
neno imara!
Msalaba
ndio asili ya mema,
Nikatua
mzigo hapo;
Nina
uzima, furaha daima,
Njoni
kafurahini papo.
2.
Kama kiti chake vivyo
Ni
yake ahadi,
Alivyowekewa
navyo
Kamwe
havirudi.
3.
Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo
lake jina!
Hataacha
roho yangu
Wala
kunikana.
4.
Atakiri langu jina,
Mbele
za Babaye,
Anipe
pahali tena
Mbinguni
nikae.
83 Kwa wingi wa nyama
1. Kwa
wingi wa nyama,
Na
sadaka pia,
Hupata
wapi salama,
Kwondoa
hatia?
2.
Sadaka ni Yesu,
Hwondoa
makosa;
Dhabihu
mwenye jina kuu,
Atanitakasa.
3. Kwa
yangu imani,
Nikuweke
sasa
Mkono
mwako kichwani
Kukiri
makosa.
4.
Roho yakumbuka
Mambo
ya mtini,
Mzigo
ulijitweka,
Ndiyo
yangu deni.
5.
Deni hutanguka,
Tukimuamini;
Kwa
damu tumeokoka,
Twimbe
furahani.
84 Niwonapo mti bora
1.
Niwonapo mti bora
Kristo
aliponifia
Kwangu
pato ni hasara
Kiburi
nakichukia.
2. Na
nisijivune, Bwana
Ila
kwa mauti yako;
Upuzi
sitaki tena,
Ni
chini ya damu yako.
3.
Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa
pendo na hamu,
Ndako
pweke hamu hiyo,
Pendo
zako zimetimia.
4.
Vitu vyote vya dunia,
Si
sadaka ya kutosha;
Pendo
zako zinawia
Nafsi,
mali, na maisha.
85 Ni mtu wa simanzi
1. Ni
“Mtu wa Simanzi”,
Mwana
wa mwenye enzi
Mwenye
mengi mapenzi!
Asifiwe
Bwana Yesu!
2.
Akawa matesoni,
“Mungu
mwana yakini
Akatoka
Mbinguni:
Asifiwe
Bwana Yesu!
3.
Akapata dhihaka,
Mzoea
– mashaka
Ndiye
yetu sadaka:
Asifiwe
Bwana Yesu!
4. Tu
wenye dhambi sana;
Kwake
dhambi hamna,
Na Mungu
twapatana:
Asifiwe
Bwana Yesu!
5.
Alikufa mtini,
Akalia
dhikini,
Sasa
yuko Mbinguni:
Asifiwe
Bwana Yesu!
6.
Punde atarejea,
Yesu
kutunyakua,
Ndipo
tutamwimbia:
Asifiwe
Bwana Yesu!
86 Damu imebubujika
1.
Damu imebubujika,
Ni ya
Imanweli,
Wakioga
wenye taka,
Husafiwa
kweli.
2.
Ilimpa kushukuru
Mwivi
mautini;
Nami
nisiye udhuru,
Yanisafi
ndani.
3.
Kondoo wa kuuawa,
Damu
ina nguvu,
Wako
wote kuokoa,
Kwa
utimilivu.
4.
Bwana tangu damu yako
Kunisafi
kale,
Nimeimba
sifa zako;
Taimba
milele.
5.
Nikifa tazidi kwimba
Sifa
za wokovu
Ulimi
ujaponyamaa
Vumbini
mwa ufu.
6.
Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa
damu yako, sehemu
Ya
mali ya kweli.
7.
Nikubali kukwimbia,
Mbinguni
milele,
Mungu
nitakusifia
Jina
lako pweke.
87 Deni ya dhambi ilimalizika
1.
Deni yangu ya dhambi,
Yesu
amelipa.
Kwake
msalabani
Nilipewa
uzima.
Deni
ya dhambi,
Msalabani,
Ilimalizikia,
Ni
huru kabisa.
2.
Bwana Yesu asema,
“Mwanangu
dhaifu,
Uwezo
wa ushindi
Hupatikana
kwangu.”
3.
Bwana, kweli naona,
Nguvu
zako pekee
Huondoa
ukoma,
Niwe
kipya kiumbe.
4.
Sina wema moyoni,
Nidai
neema,
Nakubali
kabisa,
Kwa
damu kusafiwa.
5.
Hata huko Mbinguni
Miguuni
pake,
“Yesu
alinifia,”
Nitaimba
milele.
88 Ndiyo damu ya Baraka
1.
Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa,
Kwake
Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili
hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe
katika damu, takuwa safi kabisa.
Safi
kabisa; safi kabisa!
Nioshe
katika damu;
Takuwa
safi kabisa.
2.
Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na
maumivu si haba yaliyompata chini.
Nataka
kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho
kinitakasacho, nami ni safi kabisa.
Safi
kabisa; safi kabisa!
Ndicho
kinitakasacho,
Nami
ni safi kabisa.
3.
Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi
ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu
kijitoni pako, naja naamini sasa;
Nioshe
kwa damu yako, takuwa safi kabisa.
Safi
kabisa; safi kabisa!
Nioshe
kwa damu yako,
Nami
ni safi kabisa.
89 Kwa Kalvari
1.
Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu
msalaba,
Wala
aliyenifilia,
Kwa
Kalvari.
Rehema
bure na neema,
Samaha
nalo nilipewa,
Ndipo
aliponifungua
Kwa
Kalvari.
2. Kwa
neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona
mimi mwovu,
Nikageuka
na kutubu,
Kwa
Kalvari.
3.
Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye
mfalme wa pekee sasa,
Kwa
furaha nitamwimbia,
Wa
Kalvari.
4.
Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema
ilishuswa toka juu,
Alitufanyia
wokovu
Kwa
Kalvari.
90 Aliteswa, aliteswa
1.
Aliteswa, aliteswa,
Msalabani
Yesu aliteswa,
Dhambi
zangu ameziondoa,
Mahali
pangu aliumizwa.
2.
Alikufa, alikufa,
Msalabani
Yesu alikufa,
Kwa
kifo chake nakombolewa,
Kwa
kuwa Yesu alinifia.
3.
’Kafufuka, ‘kafufuka,
Kaburini
Yesu alitoka,
Nami
nimewekwa huru pia,
kwa
kuwa Yesu alifufuka.
4.
Yuko hai, yuko hai,
Mbinguni
anaishi Mwombezi,
Daima
huniombea mimi,
Kwa kuwa
Yesu adumu hai.
5.
Atarudi, atarudi,
Siku
moja Yesu atarudi,
Na
tutamwonapo tutafurahi,
Kwa
kupelekwa kwake Mbinguni.
6.
Sifa kwake, sifa kwake,
Mbinguni
na huimbwa milele,
Kwa
furaha, masifu, na shangwe,
Tutamwimbia
Yesu milele.
91 Mapenzi yako yafanyike, Bwana
1.
Mapenzi yako yafanyike,
Wewe
mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange
upendavyo,
Mimi
tayari, naja kwako.
2.
Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji
dhambi zote,
Unisafishe
vya kimwili,
Niinamapo
Msalabani.
3.
Mapenzi yako yafanyike,
Mimi
dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo
wote, kwako kweli,
Sasa
niponye, Ee, Mwokozi.
4.
Mapenzi yako yafanyike,
Natoa
kwako vitu vyote,
Maisha,
mali, moyo, mwili,
Vyote
ni vyako, kweli, kweli.
5.
Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi
yangu yavunjike,
Ninakubali
uwe Bwana,
Ni
mali yako, twaa kabisa.
6.
Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale
siku zote,
Sura
ya Yesu umba kwangu,
Nijaze
Roho nayo nguvu.
92 Nataka nimjue Yesu
1.
Nataka nimjue Yesu,
Na
nizidi kumfahamu,
Nijue
pendo lake, na
Wokovu
wake kamili.
Zaidi,
zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue
pendo lake, na
wokovu
wake kamili.
2.
Nataka nione Yesu,
Na
nizidi kusikia,
Anenapo
kitabuni,
Kujidhihirisha
kwangu.
3.
Nataka nifahamu, na
Nizidi
kupambanua
Mapenzi
yake, nifanye
Yale
yanayompendeza.
4.
Nataka nikae naye,
Kwa mazungumzo
zaidi,
Nizidi
kuwaonyesha
Wengine
wokovu wake.
93 Bwana amefufuka
1.
Bwana amefufuka, Aleluya.
Twimbe
na malaika, Aleluya.
Sifa
zetu na shangwe, Aleluya.
Na zao
zisitengwe, Aleluya.
2.
Ukombozi timamu, Aleluya.
Umetimu
kwa damu, Aleluya.
Mshindi
asifiwe, Aleluya.
Yu hai
kwa milele. Aleluya.
3.
Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya.
Vi
wapi? Na kaburi? Aleluya.
Kifo
hakimuweki, Aleluya.
Ametoka
peponi, Aleluya.
4. Yu
hai mtukufu; Aleluya.
Cha
kifo hatuhofu! Aleluya.
Alitufia
sisi, Aleluya.
Tuwe
mahuru nasi, Aleluya.
5.
Kichwa chatangulia, Aleluya.
Tupae,
nasi, pia!, Aleluya.
Kwa
kuwa tuna fungu, Aleluya.
Mti,
kaburi, mbinguni, Aleluya.
6.
Ndiwe Mwokozi wetu, Aleluya.
Sifa
ni yako Yesu, Aleluya.
Utukuzwe
pekeo, Aleluya.
Ni
wewe ufufuo, Aleluya.
94 Siku ya mbingu kujawa na sifa
1.
Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi
zilizidi duniani;
Yesu
akaja azaliwe mtu,
Awe na
watu ulimwenguni.
Alinipenda,
alinifia,
Ameondoa
na dhambi zangu;
Alifufuka
nipewe haki,
Yuaja
tena Mwokozi wangu.
2. Na
siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza
msalabani;
Aliumia,
aliaibishwa,
Ili
atuokoe dhambini.
3.
Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini
alipumzika;
Matumaini
yetu wenye dhambi,
Ni
mwokozi, kwake twaokoka.
4.
Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe
likatoka mlangoni,
Alifufuka
kwa kushinda kwake,
Naye
yuko milele Mbinguni.
5.
Siku moja atatujia tena;
Utukufu
wake tutaona;
Atawaleta
na wapenzi wetu;
Mwokozi:
wangu, tutaonana.
95 Hivi vita vimekoma
Aleluya!
Aleluya! Aleluya!
1. Hivi
vita vimekoma,
Vimeshindwa
na uzima,
Na
asifiwe daima,
Bwana
Yesu.
2.
Nguvu za kifo ni hizo,
Ila
hazina uwezo,
Ndizo
sasa avunjazo,
Bwana
Yesu.
3.
Siku tatu za huzuni,
Kisha
atoka ufuni,
Asifiwe
duniani,
Bwana
Yesu.
4.
Mapingu ameyavunja,
Mbingu
amezifungua,
Nasi
sasa twamwimbia,
Bwana
Yesu.
5. Na
ulivyopigwa wewe,
Ni
kwamba tufunguliwe,
Milele
na usifiwe,
Bwana
Yesu.
96 Mle kaburini, Yesu mwokozi
1. Mle
kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa
chini, Bwana wangu!
Bwana!
Amefufuka,
Kifo kimeshindwa
kabisa!
Gizani
mle alitoka chini,
Sasa
atawala huko Mbinguni!
Yu
hai! Yu hai!
Bwana
Yesu yu hai!
2.
Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana
ujao, Bwana wangu!
3.
Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure
ni muhuri, Bwana wangu!
4.
Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi!
Pingu
zimevunjwa, Bwana wangu!
97 Tazameni huyo ndiye
1.
Tazameni huyo ndiye,
Mwenye
kushinda vita;
Haya,
tumsujudie;
Nyara
anazileta;
Watu
wote msifuni,
Sasa
yumo kitini.
2.
Msifuni malaika,
Mtukuzeni
sana,
Wote
waliookoka
Watamsifu
Bwana;
Watu
wote msifuni,
Sasa
yumo kitini.
3.
Walimfanya dhihaka
Zamani
wenye shari,
Kwao
waliookoka
Ni
Bwana wa fahari;
Watu
wote msifuni.
Sasa
yumo Kitini.
4.
Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni
nyimbo za sifa kuu,
Za
Bwana Yesu kitini,
Kutawazwa,
yeye tu;
Watu
wote msifuni
Sasa
yumo Kitini.
98 Huyo ndiye anashuka
1.
Huyo ndiye! anaskuka,
Aliyetufilia,
Wengi
waliookoka,
Wakimfurahia,
Aleluya!
Yesu
aturudia.
2.
Sote tutamtazama,
Amekaa
kitini,
Nao
waliomcoma,
Kumkaza
mtini,
Na
kilio, wamuone enzini.
3.
Alama za kifo chake
Hata
sasa anazo
Na
waaminifu wake
Wapendezewa
nazo.
Alipata,
Kwetu
alama hizo.
4.
Wokovu utakiwao
Sasa
wapatikana,
Na
watakatifu hao
Mbinguni
wakutana
Kumlaki,
Ndiyo
siku ya Bwana
5.
Wakusujudie wote
Mbele
ya kiti chako.
Zako, Bwana,
nguvu zote
Itwae
milki yako
Njoo
Bwana,
Sisi
tu watu wako.
99 Maelfu na maelfu
1.
Maelfu na maelfu
Wenye
nguo bora!
Masafu
ya waongofu
Wenye
na bendera!
Amekwisha
kamili
Vita
vya shetani
Fungueni
lango hili;
Njoni,
ingieni!
2.
Imbeni aleluya,
Zipae
Mbinguni!
Pigeni
sana sauti
Kwa
kutumaini!
Kwa
hiyo viliumbwa
Nchi
hata Mbingu
Dhiki
za muda zikisha,
Asifiwe
Yesu.
3.
Loo! Tukionana
Pwani
ya ng’amboni!
Loo!
Tukishirikiana
Milele
Mbinguni!
Midomo
yote pia,
Huko
itaimba
Wajane
kufufukiwa
Na
kila yatima!
4.
Himiza enzi yako,
Uliyetufia
Utimize
watu wako,
Wakosaji
pia,
Mpendwa
wa taifa
twakutumaini!
Uzifunue
ishara
Urudi
enzini!
100 Tumrudie Bwana
1.
Mbona washangaa njiani?
Mbona
warejea nyuma?
Warudi
tena gizani
Alimokutoa
Bwana?
2. Ni
ya bure yote haya,
Uliyofunzwa
ya Mungu?
Ni
bure amekufia
Bwana
Yesu kwa uchungu?
3.
Wamtia kristo aibu
Na
maneno yake pia?
Siku
yaja ya hesabu,
Utamjibuje
Bwana?
4.
Upandapo tena hayo,
Halafu
utayavuna.
Rudi
kwa Bwana upesi,
Mwombe
akupokee tena.
101 Twonane milele
1.
Nyimbo na tuziimbe tena
Za
alivyotupenda mbele;
Kwa
damu ya thamani sana!
Mbinguni
twonane milele.
Twonane
milele,
Twonane
bandarini kule;
Twonane
milele,
Twonane
bandarini kule.
2.
Hupozwa kila aoshwaye,
Kwa
damu ya Kondoo yule;
Ataishi
afurahiye
Vya
Yesu mbinguni milele.
3.
Hata sasa hufurahia
Tamu
yake mapenzi yale,
Je,
kwake tukifikilia,
Kutofarakana
milele?
4.
Twende mbele kwa jina lake,
Hata
aje mwokozi yule,
Atatukaribisha
kwake,
Tutawale
naye milele.
5. Sauti
zetu tuinue
Kumsifu
Mwokozi yule,
Ili
watu wote wajue
Wokovu
u kwake milele.
102 Kazi yangu ikiisha
1.
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na
kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua
Mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa
wa kwanza kunilaki.
Nitamjua,
nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua,
nitamjua, kwa alama za misumari.
2.
Furaha nitapata nikiona makao
Bwana
aliyotuandalia;
Nitamsifu
mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa
pahali Mbinguni.
3. Nao
waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona
tena huko juu;
Lakini
nifikapo kwake huko Mbinguni,
Nataka
kumwona Mwokozi kwanza.
4.
Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo
machozi wala huzuni.
Nitauimba
wimbo wa milele; lakini
Nataka
kumwona Mwokozi kwanza.
103 Kaa nami
1. Kaa
nami, ni usiku tena;
Usiniache
gizani, Bwana;
Msaada
wako haukomi;
Nili
peke yangu, kaa nami.
2.
Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni
la kunifurahisha;
Hakuna
ambacho hakikomi,
Usiye
na mwisho kaa nami.
3.
Nina haja nawe kila saa;
Sina
mwingine wa kunifaa;
Mimi
nitaongozwa na nani
Ila
wewe? Bwana, kaa name.
4.
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo
lote, si taabu;
Kifo
na kaburi haviumi;
Nitashinda
kwako, kaa nami.
5.
Nilalapo nikuone wewe,
Gizani
mote nimulikiwe;
Nuru
za mbinguni hazikomi,
Siku
zangu zote kaa nami.
104 Twasoma ni njema sana
1.
Twasoma, ni njema sana
Mbinguni,
kwa Bwana;
Twasoma,
dhambi hapana,
Mbinguni
kwa Bwana;
Malaika
wema wako,
Vinanda
vizuri viko,
Na
majumba tele yako,
Mbinguni
kwa Bwana.
2.
Siku zote ni mchana,
Ni
nchi ya raha;
Wala
machozi hapana,
Ni
nchi ya raha;
Walioko
wanuona
Uso wa
Mwokozi, tena
Jua
jingine hapana,
Ni
nchi ya raha.
3.
Nyama na vitu viovu
Havimo
kabisa;
Kifo
nacho, na ubovu,
Havimo
kabisa.
Ni
watakatifu wote,
Wameoshwa
dhambi zote;
Wasiosafiwa
wote
Hawamo
kabisa.
4. Tuna
dhambi, pia sote,
Mwokozi
akafa;
Kwake
tutaoshwa zote,
Mwokozi
akafa;
Kwake
twapata wokovu,
Tutawona
utukufu;
Mbinguni
tutamsifu;
Mwokozi
akafa.
5.
Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni
kwa Bwana;
Huku
chini sio kwetu,
Twendeni
kwa Bwana;
Tusishikwe
na…
105 Kuwatafuta
1.
Kuwatafuta wasioweza,
Kuomba
wamrejee Yesu,
Kuwaambia
maneno yake,
“Njooni
kwangu, nawapenda”.
Nitakwenda,
(kwenda), niwatafute
Waongofu
(wa Bwana) wageuke,
Waingie
(wote) katika zizi
La
Mkombozi (wetu) Yesu kristo.
2.
Kuwatafuta wasioweza,
Waonyeshwe
Mwokozi wetu,
Kuwaongoza,
wapate wote
Uzima
wa milele.
3.
Kazi hiyo nataka kufanya,
Leo
nimesikia mwito
Kuwainua
waangukao,
Waletwe
kwake Yesu njia.
106 Mungu awe nanyi daima
1.
Mungu awe nanyi daima,
Hata
twonane ya pili,
Awachunge
kwa fadhili,
Mungu
awe nanyi daima.
Hata
twonane huko juu,
Hata
twonane kwake kwema;
Hata
twonane huko juu,
Mungu
awe nanyi daima.
2.
Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike
mbawaze,
Awalishe,
awakuze;
Mungu
awe nanyi daima.
3.
Mungu awe nanyi daima;
Kila
wakati wa shani
Awalinde
hifadhini;
Mungu
awe nanyi daima.
4.
Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie
sana,
Awapasulie
kina;
Mungu
awe nanyi daima.
107 Ewe Baba wa Mbinguni
1.
Ewe, Baba wa Mbinguni,
Usikie
twombalo
Hapa
chini duniani,
Na uwe
radhi nalo
Ee
Mungu, bariki
Ndugu
hawa wawili!
Ee
Mungu, bariki
Ndugu
hawa wawili!
2.
Watu hawa mbele zako,
Na
mbele ya kanisa;
Watimize
Neno lako
Wanakutana
sasa.
3.
Kama Yesu na Kanisa,
Ni
mmoja, na hivyo,
Watu
hawawape sasa
Wawe
mmoja vivyo
4. Walinde,
Bwana, daima,
Wabariki
nyumbani
Uwape
nyingi salama
Humu
ulimwenguni.
5.
Wabariki, ewe Bwana,
Watu
hawa wawili,
Wape
upaji wa wana,
Wafurahishwe
kweli.
6.
Siku za duniani
Zitakapopungua,
Wape
kurithi Mbinguni
Mema
ya kwendelea.
108 Twenenda sayuni
1.
Mpendao Bwana
Ije
raha yenu!
Imbeni
nyimbo za raha
Wa
ibada yenu.
Twenenda
Sayuni,
Mji
mzuri Sayuni;
Twenenda
juu Sayuni
Ni
maskani ya Mungu.
2.
Wasiimbe wao
wasioamini,
Watoto
wa Mungu ndio
waimbao
chini.
3.
Twaona rohoni
Baraka
za Mungu,
Tusijafika
Mbinguni
Kwenye
utukufu.
4.
Tutakapo mwona
Masumbuko
basi,
Huwa
maji ya uzima,
Anasa
halisi.
5.
Tupaaze sauti,
Na
fute machozi,
Twenenda
kwa Imanweli
Naye
ni Mwokozi.
109 Nitaimba ya Yesu
1.
Nitaimba ya Yesu,
Kwa
rehema zake,
Baraka
nyingi sana
Nimepata
kwake;
Nitaimba
ya Yesu,
Sadaka
ya Mungu,
Alimwaga
damu
Ukombozi
wangu.
2.
Nitaimba ya Yesu
Hapa
siku zote,
Nitakapokumbuka
Vyema
vyake vyote;
Nitaimba
ya Yesu
Hata
mashakani,
Yeye
atanilinda
Mwake
ubavuni.
3.
Nitaimba ya Yesu
Niwapo
Njiani;
Takaza
Mwendo, hata
Nifike
Mbinguni;
Nikiisha
ingia
Mlangoni
mle,
Yesu
nitamwimbia
Mbinguni
milele.
110 Mapya ni mapenzi hayo
1.
Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi
tunayo,
Saa za
giza hulindwa
Kwa
uzima kuamshwa.
2.
Kila siku, Mapya pia
Rehema,
wema, na afya,
Wokofu,
na msamaha,
Mawazo
mema, furaha.
3.
Tukijitahidi leo
Na
mwendo utupasao,
Mungu
atatueleza
Yatakayompendeza.
4.
Mambo yetu ya dunia
Mungu
atayang’aria,
Matata
atageuza
Yawe
kwetu ya Baraka.
5.
Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia,
Yatosha:
tutafaidi
Huvuta
kwake zaidi.
6. Ewe
Bwana, siku zote,
Tusaidie
kwa yote:
Mwendo
wetu wote vivyo,
Uwe
kama tuombavyo.
111 Neno lako Bwana
1.
Neno lako, Bwana,
Ni
imara sana;
Lilo
latwongoza,
Lilo
latufunza.
2.
Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno
lake Bwana
Ni
ulinzi sana.
3.
Siku za dhoruba
Soma
ukiomba;
Neno
lake Bwana
Msaada
sana.
4.
Ukiliamini,
Hwenda
na amani;
Una na
furaha
Neno
ni siraha.
5. Ni
furaha kweli,
Na
wingi wa mali,
Neno
lake Bwana
Kwa
wasiokana
6.
Neno la rehema,
Tukali
wazima;
Faraja
I papo,
Tufarikanapo.
112 Nilikupa wewe maisha yangu
1.
Nilikupa wewe
Damu
ya moyoni,
Ili
wokolewe,
Winuke
ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa
nini?
2.
Nilikupa miaka
Yangu
duniani
Upate
inuka,
Kuishi
Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa
nini:
3.
Niliacha nuru
Za
Baba, Mbinguni,
Kwingia
taabu
Za
ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa
nini?
4.
Niliteswa sana,
Mateso
kifoni,
Usije
yaona
Hayo
ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa
nini?
5.
Nimekuletea
Huku
duniani
Upendo
na afya
Zatoka
Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa
nini?
6.
Nipe siku zako,
Udumu
mwangani;
Na
taabu yako,
Wingie
rahani
Nafsi,
pendo, mali,
Twae
Imanweli.
113 Ni mfalme wa mapenzi
1. Ni
Mfalme wa mapenzi
Ndiye
anichungaye,
Sipungukiwi,
hawezi.
Kunipoteza
yeye.
2. Kando
ya mji mazima
Yeye
huniongoza
Katika
malisho mema
Daima
hunilaza.
3.
Mara nyingi hupotea
Kwa
ukaidi wangu,
Naye
huniandamia,
Hunirudisha
kwangu.
4.
Uvulini mwa mauti,
Siachi
hatari kamwe,
Wewe
Bwana huniachi,
Mwokozi
wangu wewe.
5.
Waniandikia meza
Neema
kwako tele.
Kwa
wewe, yote naweza.
Na
msalaba mbele.
6.
Kamwe hautapungua
Uule
wema wako;
Mwisho,
atanichukua,
Juu,
niimbe kwako.
114 Bwana Mungu, nashangaa kabisa
1.
Bwana Mungu, nashangaa kabisa
Nikitazama
kama vilivyo
Nyota,
ngurumo, vitu vingi vyote
viumbwavyo
kwa uwezo wako.
Roho
yangu na ikuimbie
Jinsi
Wewe ulivyo Mkuu,
Roho
yangu na ikuimbie
Jinsi
Wewe ulivyo Mkuu.
2.
Nikitembea pote duniani,
Ndege
huimba, nawasikia,
Milima
hupendeza macho sana,
Upepo
nao nafurahia.
3. Nikikumbuka
kama Wewe Mungu
Ulivyompeleka
Mwanao,
Afe
azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua
ni vigumu mno.
4.
Yesu Mwokozi utakaporudi
Kunichukua
kwenda Mbinguni,
Nitashukuru
na kwimba milele,
Wote
wajue jinsi ulivyo.
115 Kilima kando ya Mji
1.
Kilima kando ya mji
Alikufa
Bwana;
Kuokoa
wakosaji
Akateswa
sana.
2.
Kabisa hayasemeki,
Mateso
dhaifu
Alikufa
mwenye Haki
Tupate
wokovu.
3.
Alimwaga damu yake
Ili
tuwe wema,
Tufae
kukaa kwake
Mbinguni
daima.
4.
Hatuna mwenye imani
Aliye
na haki,
Wa
kutosha yetu deni,
Rafiki
Yesu tu.
5.
Alijua peke yake
Kufungu
Mbingu
Ufunguo
damu yake
Kondoo
wa Mungu.
6.
Aliyetupenda hivyo
Nasi
tumpende,
Tukamtumai
vivyo
Na
kazi tutende.
116 Bwana , U sehemu yangu
1.
Bwana u sehemu yangu,
Rafiki
yangu wewe;
Katika
safari yangu
Tatembea
na wewe;
Pamoja
na wewe,
Pamoja
na wewe,
Katika
safari yangu
Tatembea
na wewe.
2.
Mali hapa sikutaka,
Ili
niheshimiwe,
Na
yanikute mashaka
Sawa
sawa na wewe,
Pamoja
na wewe,
Pamoja
na wewe,
Heri
nikute mashaka
Sawasawa
na wewe.
3. Niongoze
safarini,
Mbele
unichukue
Mlangoni
kwa Mbinguni
Niingie
na wewe.
Pamoja
na wewe,
Pamoja
na wewe,
Mlangoni
kwa mbinguni,
Niingie
na wewe.
117 Tufani inapovuma
1.
Tufani inapovuma
Sana
moyoni mwangu,
Huona
pa kujificha
Mkononi
mwa Mungu.
Hunificha,
hunificha
Adui
hatanipata,
Hunificha,
hunificha,
Mkononi
mwake.
2.
Pengine kuna taabu
Yanisongeza
kwake;
Naijua
si hasira,
Ni ya
mapenzi yake.
3.
Adui wakiniudhi
Nami
nikisumbuka,
Mungu
atavigeuza
Vyote
viwe baraka.
4.
Niishipo duniani
Ni
tufani daima,
Anilindapo
rohoni
Nitakaa
salama.
118 Ni ujumbe wa Bwana
1. Ni
ujumbe wa Bwana, Aleluya!
wa
maisha ya daima,
Amenena
mwenyewe, Aleluya!
Utaishi
ukitazama.
Tazama,
ishi sasa!
Kumtazama
Yesu,
Amenena
mwenyewe, Aleluya!
Utaishi
ukitazama.
2. Ni
ujumbe wa wema, Aleluya!
Nawe
shika, rafiki yangu!
Ni
habari ya raha Aleluya!
Mwenye
kuinena ni Mungu.
3.
Uzima wa daima,Aleluya !
Kwake
Yesu utauona.
ukimtazama
tu, Aleluya!
Wokovu
u pweke kwa Bwana.
119 Si damu ya nyama
1. Si
damu ya nyama
Iliyomwagika
Iwezayo
kuondoa
Dhambi
za wakosa.
2.
Yeye Bwana Yesu
Sadaka
ya Mungu,
Mwenye
damu ya thamani,
Ni
mwokozi kweli.
3. Kwa
imani yangu,
Namshika
yeye,
Naziweka
dhambi zangu
Juu ya
kichwa chake.
4.
Mzigo wa dhambi
Sichukui
tena,
Ameuchukua
yeye,
Juu ya
msalaba.
5.
Bwana Yesu ndiye,
Mwokozi
wa kweli
Tumsifu
siku zote,
Twapata
uhuru.
120 Enyi wanadamu
1.
Enyi wanadamu mbona
Sana
mwatanga-tanga,
Kama
kondoo wanyonge,
Wasio
na mchunga?
Yuko
mchunga mmoja
Mwenye
mapenzi mema;
Haya
kutaneni kwake,
Atawachunga
vyema.
2.
Mungu tunamwona kuwa
Mwenye
uwezo wote;
Na
nguvu zake zapita
Mawazo
yetu yote:
Ni
Baba,mapenzi yake
Ni
makubwa hakika;
Hatuwezi
kuyajua,
Na
hayana mpaka.
3.
Rehema za Mungu nazo
Zina
upana sana;
Kama
huo wa bahari,
Mwisho
wake hapana;
Haki
yake ina mema,
Kwa
hayo twashukuru,
Kwetu
uko msamaha,
Furaha
na uhuru.
4.
Mapenzi yake mapana,
Sisi
hatuna cheo
Cha
kutosha, nao moyo
Una
wema upeo;
Ukombozi
mwingi mno
Katika
damu yake;
Sote
twapata furaha,
Kwa
maumivu yake.
5. Yesu
mkaribieni
Njoni
msife myoyo;
Njoni
kwake kwa imani,
Mema
yake ni hayo;
Heri
tuwe kama wana
Tush…
121 Liko lango moja wazi
1.
Liko lango moja wazi,
Ni
lango la mbinguni;
Na
wote waingiao
Watapata
nafasi.
Lango
ndiye Yesu Bwana
Wote
waingie kwake,
Lango!
Lango
La
Mbinguni ni wazi.
2.
Yesu ndiye lango hili,
Hata
sasa ni wazi,
Kwa
wakubwa na wadogo,
Tajiri
na maskini.
3.
Hili ni lango la raha,
Ni
lango la rehema;
Kila
mtu apitaye
Hana
majonzi tena.
4.
Tukipita lango hili
Tutatua
mizigo,
Tuliochukua
kwanza,
Tutavikwa
uzima.
5.
Hima ndugu tuingie
Lango
halijafungwa,
Likifungwa
mara moja
Halitafunguliwa.
122 Bwana Yesu
1.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona
unaumia? Unateseka sana,
Kwa
ajili ya kuomba,
Waomba
na jasho jingi likageuka damu.
Kumbe!
Ni dhambi zangu zinazokuumiza.
Bwana
wangu, Mungu wangu,
Mimi
leo, naja kwako
Ili
niziungame.
2.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona
unaumia, na mizigo mizito?
Umejitwalia
wewe, msalaba mabegani
Kwa
ajili ya watu.
3.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona
unatukanwa, wawambwa kama mwizi,
Bila
kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe,
Chukua
roho yangu.
4.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Muda
ulipofika, nchi ikawa giza,
Mbinguni
pakatulia,
Angani
pakawa kimya,
Watu
wakaogopa.
5.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Jinsi
ulivyoumwa, ukamwomba Baba,
Leo
umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni,
Naimba,
Haleluya.
123 Nimeketi mimi nili kipofu
1.
Nimeketi mimi nili kipofu
Gizani
nangojea macho;
Ewe
Bwana Yesu mwenye wokovu,
Ondoa
dhambi zangu nzito.
Huruma
hakuna aonaye,
Gizani
nagojea macho,
Sasa
nitakase nikusihiye,
Yesu,
na dhambi zangu nzito.
2.
Tangu siku nyingi nimepofuka
Natamani
uso nikwone;
Ewe
Bwana Yesu, mwenye baraka
Sema
neno, basi, nipone.
3.
Nimeketi mimi nili na giza,
Nami
ya kutumai sina;
Ili
nasikia kunong’oneza,
“Kwake
Yesu kuna kupona.”
124 Mungu ulisema
1.
Mungu ulisema,
Giza
ilikoma;
Twakushukuru!
Twakusihi
sote,
Duniani
mote
Na kwa
watu wote,
Iwe
nuru.
2.
Yesu ulikuja,
Ulituletea
Nuru
kuu;
Macho
kwa vipofu,
Maisha
kwa wafu;
Twakushukuru.
3.
Roho kiongozi,
Roho
wa mapenzi
Tia
nuru;
Mwovu
hata sasa
Watu
huwatosa,
Tunakwomba
hasa,
Iwe
nuru.
4.
Mungu wa utatu
Mwanga
wao watu,
Tuwe
huru;
Twende
kote-kote
Wafundishwe
wote,
Duniani
mote,
Iwe
nuru.
125 Ati twonane Mtoni?
1. Ati
twonane mtoni?
Maji
mazuri ya Mbingu;
Yanatokea
mwangani,
Penye
kiti cha Mungu.
Naam,
twonane mtoni!
Watakatifu,
kwenu ni mtoni!
Tutakutanika
mtoni
Penye
kiti cha Mungu.
2.
Tukitembea mtoni
Na
Yesu mchunga wetu
Daima
tu ibadani
Usoni
pake kwetu.
3.
Kwang’ara sana mtoni
Cha Mwokozi
ni kioo,
Milele
hatuachani,
Tumsifu
kwa nyimbo.
4. Si
mbali sana mtoni,
Karibu
tutawasili,
Mara
huwa furahani
Na
amani ya kweli.
1. Ni
mji mzuri,
Mbali
sana;
Watu
wanawiri
Kama
jua;
Waimba
kwa tamu,
Tuna
wema hakimu:
Sifa
na idumu,
Kwake
Bwana.
2. Ni
mji mzuri
Twende
sote!
Una na
fahari
Msikawe!
Raha
tutaona,
Dhambi
hapana tena;
Hatutaachana
Siku
zote.
3. Ni
mji mzuri;
Macho
yote
Huko
wanawiri
Kama
pete;
Baba
tutamwona,
Tukifanywa
tu wana;
Tumo
kupendana
Naye
sote.
4. Ni
mji mzuri;
Tusipotee
Na
tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze,
tutume
Kwa
taji na ufalme:
Sifa
na zivume
Siku
zote.
127 Bwana Yesu atakuja
1.
Bwana Yesu atakuja, Vumilia!
Omba,
ukiwa na haja, Vumilia!
Mbingunu
Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako,
Nawe
utafika huko, Vumilia!
2.
Ikikucheka dunia, Vumilia!
Mwovu
atakuvizia, Vumilia!
Hataweza
kukushinda, Bwana Yesu akulinda,
Roho
yako, akupenda, Vumilia!
3. Na
ukiwa hatarini, Vumilia!
Dhiki
nyingi duniani, Vumilia!
Vyatupasa
kuyakuta, Majaribu na matata,
Na
Bwana hakutuficha; Vumilia!
4.
Adui wakikutana, Vumilia!
Na
ndugu wakikukana, Vumilia!
Zote,
zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha
Mungu
chini atashusha; Vumilia!
5.
Moyoni una majonzi, Vumilia!
Ndiyo
bonde-ya-machozi, Vumilia!
Hima
tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana
Tena
hatutaachana; Vumilia!
128 Mmoja apita wote
1.
Mmoja apita wote,
Atupenda;
Zaidi
ya ndugu wote,
Atupenda;
Rafiki
wa duniani,
Wote
hatuwaamini;
Yesu
kwa kila zamani,
Atupenda.
2.
Kumjua ni uzima,
Atupenda;
Jinsi
ajaavyo wema
Atupenda;
Yeye
ametununua
Kwa
damu aliyomwaga,
Dhambini
kutuokoa,
Atupenda.
3.
Sasa tunaye rafiki,
Atupenda;
Hupenda
kutubariki;
Atupenda;
Twapenda
kumsikia,
Atwita
kukaribia,
Nasi
tutamwamania,
Atupenda.
4.
Husamehe Dhambi zetu,
Atupenda;
Hushinda
adui zetu,
Atupenda;
Anatwonea
huruma,
Hatupati
ila mema,
Anatwongoza
salama,
Atupenda.
129 Karibu na wewe
1.
Karibu na wewe,
Mungu
wangu
Karibu
zaidi,
Bwana
wangu
Siku
zote niwe
Karibu
na wewe,
Karibu
zaidi
Mungu
wangu.
2.
Mimi nasafiri
Duniani,
Pa
kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo
niwe
Karibu
na wewe,
Karibu
zaidi
Mungu
wangu.
3. Na
kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba,
uwe maji
Ya
wokovu;
Mashakani
niwe
Karibu
na wewe;
Karibu
zaidi
Mungu
wangu.
4. Na
nyumbani mwa juu,
Baba yangu,
Zikikoma
hapa
Siku
zangu,
Kwa
furaha niwe
Pamoja
na wewe,
Karibu
kabisa
Mungu
wangu.
130 Niongoze, Bwana Mungu
1.
Niongoze, Bwana Mungu,
Ni
msafiri chini;
Ni
mnyonge, nguvu sina:
Nishike
mkononi;
U
mkate wa Mbinguni,
nilishe
siku zote.
2. Kijito
cha maji mema,
Kitokacho
mwambani,
Nguzo
yako, moto, wingu,
Yaongoza
jangwani;
Niokoe
mwenye nguvu;
Nguvu
zangu na ngao.
3.
Nikikaribia kufa,
Sichi
neno lolote,
Wewe
kifo umeshinda
Zinawe
nguvu zote,
Tutaimba
sifa zako,
Kwako
juu milele.
131 Piga sana vita vyema
1.
Piga sana vita vyema
Kwa
ushujaa daima,
Yesu
ndiye nguvu zako,
Yesu
ndiye kweli yako.
2.
Kaza mwendo, ushindane
Angaza
macho, umwone
Yesu
ndiye njia yako,
Naye
ndiye tuzo lako.
3.
Tupa kizito, simama,
Tazama
mbele, si nyuma;
Ni yeye
uzima wako,
Naye
ni kipendo chako.
4.
Tangamka, uamini
Akushika
mikononi
Hageuki,
akupenda,
Kuwa
naye una pia.
132 Sauti sikilizeni
1.
Sauti sikilizeni
Za
waimbao juu,
“Aleluya,
Aleluya,
Aleluya,
mkuu!”
Wako
makundi-makundi
Kama
nyota wang’ara,
Kwa
makuti ya mitende,
Na
meupe wamevaa.
2.
Wazazi na manabii
Wafanyaji
wa njia;
Mashahidi,
waandishi,
Nao
wafalme pia!
Mabikira
kina-mama,
Wajane
wa kusali,
Waimba
wakikutana
“Msifunu
Imanweli”.
3.
Watu toka huzunini
Wameosha
na nguo,
Ni kwa
damu yake Yesu;
Maonjo,
mbali nao!
Walitekwa,
walikatwa
Hata
kwa misumeno,
Kwao
kifo na shetani
Walishindiwa
mno.
4.
Mungu mumo mwake Mungu,
Nuru
mumu mwa nuru,
Kwa
kufungamana mwako
Tutaishi
mahuru;
Tujalize,
Imanweli,
Kujaa
kwako wewe
Mungu
Baba, Mungu Mwana,
Mungu
Roho, tunawe.
133 Ni wako Mungu
1. Ni
wako Mungu!
Ni
furaha kwangu,
Ni
raha kumjua mwokozi wangu.
Aleluya
enzi ndako;
Aleluya,Amin.
Aleluya,enzi
ndako;
Rejea
Yesu.
2.
Mwana wa Mungu
Ndiye
fungu langu,
Na
moyo hufurahi kwa Yesu wangu.
3. Raha
ya kweli
Ina
jina hili,
Na
aliyeshika,ana Mbingu kweli.
4.
Nimeingia
Mapendano
haya,
Nimepata
uzima na Mbingu pia.
5.
Nilipo chini,
Ni
mwako kazini
Hata
nije kwako uliko Mbinguni.
134 Juu yake langu shaka
1. Juu
yake langu shaka,
Yesu
namuwekea,
Nami
sitafedheheka
Nikimtegemea.
Natumai,
natumai,
Nnatumai
kwake tu;
Natumai,
natumai,
Natumai
kwake tu.
2. Juu
yake, dhambi zangu;
Aniosha
kwa damu;
Nionekane
kwa Mungu,
Nisiye
na laumu.
3. Juu
yake yangu hofu;
Kwake
nimetulia;
Sipotei
kwa upofu
Njia
aning’azia.
4. Juu
yake raha yangu;
Humuangalia
tu;
Mwenye
kila ulimwengu,
Aniruzuku
na huu.
5. Juu
yake, moyo wangu;
Hali
yangu na mali;
Mimi
wake, Yeye wangu,
Twapasana
kamili.
135 Mapenzi ya milele
1.
Mapenzi ya milele
Ndiyo
yanipendezayo;
Yalinipenda
mbele,
Sina
fahamu nayo;
Sasa
amani yake
Tele
rohoni mwangu,
Ni
mimi kwa kuwa wake,
Na
yeye kuwa wangu,
Ni
mimi kuwa wake,
Na
yeye kuwa wangu
2.
Mbingu zinang’ara juu,
Na
nchi nayo vivyo;
Macho
ya dunia tu
Hayajaona
hivyo;
Nyuni
huimba sana,
Maua
yana rangi,
Ni
kumjua Bwana
Na
pendo zake nyingi,
Ni
kumjua Bwana
Na
pendo zake nyingi,
3.
Mambo mengi maovu
Nayo
yenye kutisha,
Sasa
hayana nguvu,
Si
yenye kututisha;
Ni
mkononi mwake,
Nalindwa
salamani
Ninajua
ni wake,
Ni
wake mapenzini.
Ninajua
ni wake,
Ni
wake mapenzini.
4.
Wake hata milele,
Si
kutengana tena;
Hunipa
raha tele
Moyoni
mwangu, Bwana;
Hiyo
nchi na Mbingu
Zitatoweka
zile,
Ni
wake, Yeye wangu,
Milele
na milele.
Ni
wak…
136 Msifuni, Yesu ndiye mkombozi
1.
Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi;
Imbeni
ya pendo zake kuu,
Sujuduni,malaika
mlioko,
Jina
lake liwe na sifa kuu.
Kama
vile mchunga uchungavyo
Vivyo
sisi kutwa atachunga.
Msifuni
mlio wakw watoto
Msifuni
aliye mchunga.
2.
Msifuni,Yesu ndiye mkombozi;
Akateswa
tupate ongoka;
Ndiye
Mwamba,Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni
kwake muangikwa,
Yesu
aliyeudhiwa na hamu
Kwa
pendo za baba yake Mungu.
Aliyefyolewa
na kusulubiwa.
Msifuni
ndilo letu fungu.
3.
Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni,enyi
malango juu;
Bwana
Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni
taji, ni yake tu.
Atakuja
kuitawala nchi,
Yesu,Mwombezi
wetu wa Mungu.
Msifuni,
ni mfalme wa salama;
Ndiye
kweli mwana wake Mungu.
137 Yesu mponya
1.
Yesu ndiye mganga wetu
Aponya
wagonjwa wote;
Mganga
wetu ni Yesu,
Aponyaye
hasira.
Tumsifu
huyo Yesu
Tumsifu
milele,
Kwani
Mponya mtakata
Mwokozi
wa wanyonge
2.
Mganga wetu ni Yesu
Huondoa
matusi;
Mganga
wetu ni Yesu,
Mwenye
kuponya choyo.
3.
Mganga wetu ni Yesu
Huponya
wivu wetu;
Yesu
ndiye aponyae
Kelele
za nyumbani.
4.
Mganga wetu ni Yesu
Mponya
wa tamaa mbaya;
Mganga
wetu ni Yesu
Uasherati
hufuta
5.
Mganga wetu ni Yesu
Aponya
kiu cha pombe,
Mganga
wetu ni Yesu
Kila
dhambi uponya
138 Tukutendereza Yesu (Luganda)
1.
Yesu, Mulokozi wange:
Lero
nze wuwo wenka;
Omusaigwo
gunazi’za
Yesu
Mwana gwendiga.
Tukutendereza,
Yesu,
Yesu
Mwana gwendiga;
Omusaigwo
gunazi’za;
Nkwebaza,
Mulokozi.
2. Eda
nafuba bufubi
Okufuna,
emirembe;
Lero
maliride dala
Okweyabiza
Yesu.
3.
Nababuliranga bantu
Obulokozi
bwona,
Obutali
bwa kitundu
Obulamba
obwobuwa
4.
Nategezanga ebya Yesu
Nobuvumunesitya;
Eyanziya
mu busibe
Nokuwonya
eyamponya.
5.
Nebaza eyanunula nze;
Eyamponya
wa kisa!
Yesu
ankuma
Ansanyusaera,
Bulijo
yebazibwe.
139 Nuru ya rohoni
1.
Nuru ya rohoni
ni
Bwana Yesu.
Nakuomba
sana
niangazishe;
ukanitazame
kwa
huruma tu,
/:
ukanitulize
mimi
maskini. :/
2.
Futa dhambi zangu
kwa
damu yako.
Hasira
ya Mungu
iniondoke.
Machubuko
yako,
hata
mateso,
/:
niyawaze vema
rohoni
mwangu. :/
3.
Nakutumaini
peke
yako tu,
niwe
mtumwa wako
pote
nilipo
utanikubali
sina
mashaka!
/:
Nitakushukuru
pasipo
mwisho. :/
140 Mahali ni pazuri
1.
Mahali ni pazuri,
ndugu
wanapokaa,
/:
wakipatana vema,
na
wakipendana. :/
2.
Kama umande mzuri,
unyweshavyo
shamba,
/:
vivyo na Mungu wetu,
hubariki
ndugu. :/
3.
Upendano hujenga,
boma
zuri kwao,
/:
wakae na amani,
waliookakoka.
:/
4. Na
ulimwengu wote,
watiwa
nuruni,
/:
halafu kundi moja,
na
mchunga mmoja tu. :/
141 Pana jito, lina maji mazuri
1.
Pana jito, lina maji Mazuri,
Yaenda
ulimwenguni.
Lametameta
nalo Linang’aa.
Walijua
jito hilo?
Ninakuita
nawe njoo!
Utafute
jito hilo!
Maji
yake yapoza Moyo.
Nawe
yateke unywe.
2.
wanywao maji haya wafurahi,
waimba
kwa shangwe kubwa.
Makosa
na shida Yanaondoshwa,
Wote
waoshwa na Bwana.
Ninakuita
nawe njoo …
3.
Jito hilo latoa maji mengi,
matamu
yapendezayo.
Yaponya
wagonjwa, Yatia nguvu,
Uchafu
watakashika.
Ninakuita
nawe njoo …
4.
maji ya jito hilo ni uzima
unaotoka
Kwa Yesu.
Damu
yake yenye kiasi kikuu
Imemwagwa
tusafike.
Ninakuita
nawe njoo …
142 Babangu kule mbiguni.
1.
Babangu kule mbinguni,
aliye
juu pa malaika,
/:aangalia
njia zangu
na
kunilinda maisha.:/
2.
Hata unywele kichwani
hauanguki
ovyo tu
/: na
siri zote za moyoni
zajulikana
kwa Baba.:/
3.
Zamani nisipojua,
amekwisha
kuandika
/:mkononi
mwake jina langu,
ndio
upedo wake mkuu.:/
4. Ee
Baba yangu u mwema,
nami
nataka kufanya
/:kama
malaika wafanyavyo
mbinguni
kwako milele!.:/
143 Nchi nzuri yametameta
1.
Nchi nzuri yametameta,
Huonekana
kule mbali,
Naye
Yesu hutuongoza.
Tukafike
na sisi huko.
/:
Sisi mbali, karibu,
Tutaimba
na sisi huko!:/
2.
Kule tutawaona wengi
Wapendwao
na Yesu Bwana,
Tutashirikiana
nao
Itakuwa
furaha kubwa.
Si
mbali..
3.
Tutamwona na Bwana Wetu,
Yesu
kristo mwokoai Wetu,
Tutashangilia
daima,
Tuna
hamu ya kwenda Kwetu.
Si
mbali..
144 Mbele ninaendelea
1.
Mbele ninaendelea,
Ninazidi
kutembea;
Maombi
uyasikie,
Ee
Bwana, unipandishe.
Ee,
Bwana, uniinue,
Kwa
imani nisimame;
Nipande
milima yote,
Ee
Bwana,
Unipandishe.
2.
Sina tamani nikae,
Mahali
pa shaka, kamwe;
Hapo
wengi wanakaa,
Kuendelea
naomba
Ee,
Bwana…..
3.
Nisikae duniani,
Ni
mahali pa shetani;
Natazamia
mbinguni,
Nitafika
na amani.
Ee,
Bwana….
145 Ndoa yetu nzima
1.
Ndoa yetu nzima
simika,
Yesu!
Usiku
na mchana
uwepo
kwetu.
Leo
tuna raha,
Wewe
watupa.
/:Ndoa
yetu Bwana
ndiwe
Baraka!/:
2.
Atoka kijana,
ataka
mchumba
siku
zinapita
za
kupimana.
Leo
twapatana
pamoja
kukaa
/:Ndoa
yetu…:/
3.
Vyote hapa chini
vinakaa
muda,
vyote
vinaoza,
tena
vyachakaa.
Pendo
la duniani
nalo
huchakaa
/:Ndoa
yetu…/:
4.
Kakaa kwetu Bwana,
kutukagua,
pendo
letu sisi
lisichakae:
Hivi
na tukae
na
baraka tu.
/:
Ndoa yetu…:/
5.
Kana arusuni
ulialikwa,
walivyoishiwa
ukaongeza,
nasi
shida zetu
utazishinda.
/:Ndoa
yetu..:/
146 Neno la Mungu takata
1.
Neno la Mungu takata
Lililotoka
mbinguni;
Ambalo
moto na panga
Haziwezi
kulishinda.
Twakushika
siku zote
Maishani
na kufani.
2.
Waliotutangulia
Waliokutegemea,
Wamekufa
mashujaa;
Nasi
tulio watoto.
Twakushika
…
3.
Neno la Mungu takata,
Tukushuhudie
nasi
Kwa
neno tamu na tendo
Kunako
wenzi au adui.
Twakushika
…
147 Tegemea mpaka kufa
1.
Tegemea mpaka kufa,
Utapata
wokovu.
Bwana
Yesu ni Mwokozi
Yeye
anakupenda.
Uje
kwake ‘sikawie’.
Yeye
akuokoa.
Njoo
upesi! Njoo upesi!
Fika
kwa Bwana Yesu.
2.
Acha mambo ya dunia
Yakuhangaishayo.
Iko
mali ya uzima
Unaitiwaa
hiyo.
Mali
hiyo ni uzima
Utapewa
na Bwana.
Njoo
upesi! …
3.
Wakatae, waepuke
Wanaokudanganya;
Na
wajinga, wakuponza,
Wakupoteza
wewe.
Ila
wewe ukatae
Kuondoka
kwa Yesu.
Njoo
upesi! …
4.
Ukijua jambo hilo
Usipolifuata
Kosa
hilo kubwa sana,
Wapasiwa
hukumu.
Vumilia,
jizuie
Utapata
uzima.
Njoo
upesi! …
5.
Bwana Yesu amekwisha
Kukutengenezea
Kitu
chema kwake Mungu,
Ndiko
unakokwenda.
Kile
kitu upendacho
Kule
utakipewa.
Njoo
upesi! …
148 Ondokeni tunaitwa
1.
Ondokeni! tunaitwa
na
walinzi wa juu mnarani
Yerusalemu,
amka wee!
Ni
usiku wa manane,
yuaja
Bwana wa arusi,
wanawali
wako wapi?
Amkeni
upesi!
Kaziwasheni
taa.
Haleluya!
Fuateni
arusini
kwenda
kumpokea Bwana!
2. Sayuni
anasikia,
moyo
waruka kwa furaha,
yu
macho anaondoka.
Mponya
wake anashuka
mbinguni
mwenye
utukufu,
aleta
mwanga wa kweli,
taji
yake yaja
na
Mwana wa Mungu.
Hosiana!
Twafuata
kwenye shangwe
tukale
karamu yake.
3.
Waimbiwa nyimbo nzuri
kwa
misemo ya watu wote
na ya
malaika mbinguni.
Tukifika
mjini kwako
kwenye
milango ya malulu
tutakuimbia
nasi.
Furaha
kama hii
haijasikiwa
duniani.
Nasi
sasa tunaimba,
tunakusifu,
Ee Bwana.
149 Haya umati wa Yesu
1.
Haya, umati wa Yesu,
Ulioungwa
naye!
Haya, enendeni
hima
Katika
vita kubwa!
Shetani
tayari,
Kupigana
na sisi!
2.
Tumfuate Yesu Kristo,
Tumwamini
yeye tu.
Mwovu
akituvizia
Sisi
hatuogopi.
Majeshi
ya mbingu
Ni
pamoja na sisi!
3.
Tukikesha na kuomba
Yesu
anayotaka,
Tukishika
neno lake
Na kumtegemea
Kwa
nguvu hizi tu
Tutaweza
kushinda!
4.
Sasa haya wenzi wangu,
Tumfuate
Yesu tu!
Siku
za maisha yetu,
Tuwe
katika yeye.
Tuache
dunia
Kuingia
mbinguni!
5.
Pale Mungu atawapa
Taji
walioshinda,
Wapate
urithi wao
Nyumbani
mwa milele.
Hayani!
Tuimbe,
Tumsifu
Bwana wetu!
150 Haya ee moyo wangu
1.
Haya ee moyo wangu,
imba
kwa furaha.
Umwimbie
Muumbaji
mbingu
na dunia.
Atukuzwaye
pote
umsifu
na wewe
kwa
nguvu zako zote,
umri
wako wote.
2.
Mungu wake Yakobo.
ndiye
Mungu wwetu.
Ukimchagua
yeye,
una
fungu jema,
unacho
kitu chema,
umepata
mali;
moyo
utakung’aa
shida
zitakwisha.
3. Ni
mwenye nguvu nyingi,
hana
amshindaye,
kwa
hekima aumba
vyote
ni ajabu,
misitu
na mabonde,
milima,mashamba,
vilivyo
baharini
wanyama
porini.
4. Ana
mizungu mingi,
kuponya
wanawe.
Anawapa
riziki,
hata
siku za njaa.
Wenye
chakula haba
wanenepa
miili:
hata
waliofungwa
anawafungua.
5.
Mashangilio yote
hayamtoshi
yeye.
Ni
mwema peke yake
nami
ni vumbi tu!
Ananihurumia
kwa
kuwa ni wake,
kwa
hiyo nalikuza
Jina
lake pote.
151 Usiku mtakatifu
1.
Usiku mtakatifu!
Wengine
walala
Wakeshao
ni Yosefu tu
na
Maria waliomlinda
Yesu
mwana mzuri
Yesu
mwana mzuri
2.
Usiku mtakatifu!
Wachunga
wapewa
habari
nzuri na malaika,
zienezwe
popote sasa:
Yesu
Mponya kaja
Yesu
Mponya kaja.
3.
Usiku mtakatifu!
Siku
ya furaha
imetuangaza
Kimungu
tumepewa
ukombozi
Kristo
amefika
Kristo
amefika.
152 Uliyesulibishwa
1.
Uliyesulubishwa,
Mtakatifu
Bwanangu,
Uwe
ngao shidani,
uniombee
mimi.
Uliyesulubishwa,
Mtakatifu
Bwanangu!
2.
Wongofu sina hata,
niondolee
makosa.
Mwovu
akinishtaki
nasumbuka
rohoni.
Wongofu
sina hata,
niondolee
makosa.
3.
Wewe tu nipokee,
nakukumbilia
wee.
Hata
nifanye bidii,
nikatoe
machozi.
Wewe
tu nipokee,
nakukimbilia
wewe
4. Uwe
ngao shidani,
Niombee
na mimi!
Hapa
nikiumizwa,
Saa ya
mwisho ikija:
Uwe
ngao shidani,
Niombee
na mimi!
153 Nimepita
ulimwengu
1.
Nimepita ulimwengu,
ulimwengu
ni mzuri,
lakini
natamani
ulimwengu
mwingine.
2.
Nimeona watu wengi,
hutafuta
daima
Maisha
yao yote,
ndiyo
taabu na shida.
3.
Imebaki hali njema
ya
furaha ya roho:
Hubirini
popote;
taabu
itatulia.
4.
Msalabani pa Golgota
jerahani
mwa Yesu
ni
mahali penye raha
kwao
wote kabisa.
154 Bariki yote yawe mema
1.
Bariki yote yawe mema,
yote
yawe mbaraka.
Watu
wa nchi za duniani,
uwajaze
utukufu.
Kaa
kwetu, Bwana, bariki.
Uamini
wee ee ndugu
kweli
yake Kristo.
Jaa
utukufu wa Bwana
siku
zako zote.
/:Vaa
Mwokozi ee
na
kweli yake, Haleluya.:/
2.
Nyumba za wote zibariki
kwa
Jina lako takata.
Ujaze
utukufu wako,
nchi
zote dunia,
Kaa
kwetu, Bwana…
3.
Nyosha mkono ubariki,
waliojiunga
nawe.
Wakupokee
maishani,
watunzwe
nawe milele.
Kaa
kwetu, Bwana…..
4.
Bwana yatunze mambo yote
yaliyo
mazuri kwako
Uwape
wote wakuombao,
wafanikishe
maisha.
Kaa
kwetu Bwana….
155 Hapana rafiki kama Yesu
1.
Hapana rafiki kama Yesu,
Yu
pekee, Yu pekee;
Hapana
mpozi kama Yesu
Yu
pekee, Yu pekee.
Yesu
ajua shida zetu,
Aweza
kutuongoza;
Hapana
rafiki kama Yesu,
Yu
pekee yu pekee.
2.
Yeye anaye sifa, ni Yesu
Yu
pekee, yu pekee;
Ndiye
aliye mnyenyekevu
Yu
pekee, yu pekee;
Yesu
ajua……
3.
Yesu pamoja nasi daima,
Yu
pekee, yu pekee;
Kwa
usiku aleta salama,
Yu
pekee, yu pekee;
Yesu
ajua……
4.
Kulinda Yesu yu Mwaminifu,
Yu
pekee, yu pekee;
Atawakubali
wahalifu,
Yu
pekee, yu pekee;
Yesu ajua…..
5.
Alipelekwa awe mwokozi,
Yu
pekee, yu peee;
Anatutayarisha
enzi
Yu
pekee, yu pekee;
Yesu
ajua…….
156 Bwana Yesu yuko wapi
1.
Bwana Yesu yuko wapi,
Mpenzi
wangu rafiki?
Njia
gani amekwenda?
Nitamwonaje
mimi?
Roho
yangu yajutishwa
Na
dhambi na huzuni;
Yesu
mpenzi wangu Mwema
Namtafuta
kwa bidii.
2.
Ninapaza sauti yangu
Nalia:wapi
Yesu?
Ndani
mwangu sina raha
Mpaka
nimwone Yesu.
Ningekuwa
na mabawa
Ningeruka
upesi
Milimani,
mabondeni
Kumtafuta
Bwanangu
3.
Aondoa shida zangu,
Maharibifu
yote.
Nikiona
taabu mimi
Anituliza
yeye.
Nitafanya
bidii sana;
Kumtafuta
popote;
Sitachoka
kutembea
Mchana
hata usiku.
4.
Bwana Yesu nitokee,
Roho
inakuita.
Niondoe
na maovu
Yesu
mwokozi wangu.
Utilize
hamu yangu
Kaa
kwangu daima.
Nikupende
sana wewe,
Niwe
wako milele.
157 Kijito cha utakaso
1.
Kijito cha utakaso
ni
damu ya Yesu,
Bwana
anao uwezo
kunipa
wokovu
Kijito
cha utakaso,
Nizame
kuoshwa humo
Namsifu
Bwana kwa hiyo
Nimepata
utakaso
2.
Viumbe vipya naona;
damu
ina nguvu,
meharibu
uovu
ulionidhulumu
3.
Naondoka kutembea
nuruni
mwa mbingu,
Na
moyo safi kabisa
kumpendeza
Mungu.
4. Ni
neema ya ajabu
kupakwa
na damu;
na
Bwana Yesu kumjua
Yesu
wa Msalaba.
158 Aniongoza po pote
1.
Aniongoza popote
NimwandameSiku
zote
Mapenzi
yake ni heri
Yalitimizwa
kalvari.
2.
Nitaongozwa na Bwana
Usiku
kucha na mchana
Yesu
rafiki wa heri
Ninakumbuka
kalvari.
3.
Lanitosha neno lake
Nishikwe
na mkono wake
Mapenzi
yake ni heri
Yalitimizwa
kalvari
4.
Nitaendelea mbele
Pamoja
naye milele
Pendo
lake ni hiyari
Bwana
Yesu wa Kalvari
159 Ushirika mkuu, furaha yangu
1.
Ushirika mkuu, furaha yangu,
Kumtegemea
Bwana Yesu,
Nina
baraka, amani pia,
Kumtegemea
Bwana Yesu.
Raha,
Raha,
Nina
raha na salama,
Raha,
Raha,
kwa
kumtegemea Yesu.
2. Ni
halisi kutembea naye,
Kwa
kumtegemea Yesu.
Naona
nuru njiani mwangu,
Kumtegemea
Bwana Yesu.
3.
Sioni shaka wala hasara,
Kumtegemea
Bwana Yesu;
Nina
amanikwake Mwolozi,
Kumtegemea
Bwana Yesu.
160 Jioni moyo wangu wakutafuta
1.
Jioni moyo wangu
wakutafuta
Bwana,
na
kukushukuru.
Unikazie
macho
yenye
baraka nyingi,
ung’aze
mwili na roho.
2.
Natumaini tena
rehema
yako Baba
hata
usiku huu.
Fukuza
majaribu
na
hila ya shetani,
ukiwa
karibu yangu
3.
Unanipenda sana,
wakaa
pamoja nami,
wanikaribisha.
Unanifurahisha
kwa
wema wako
mwingi,
sababu
hii nakusifu.
4.
Maisha yanapita upesi,
ni
safari ya kwenda
mbinguni.
Unifundishe,
Bwana,
kuelekea
kwako:
Pazuri
ni mbinguni tu.
161 Usiku uingiapo
1.
Usiku uingiapo,
umwaze
Mungu Mkuu,
aendeshaye
dunia
kwa
mwendo mtulivu.
2. Kwa
nini wahangaika
usiku
namchana?
Umtwishe
huzuni yako
aliyekuumba.
3.
Kwake haujapunguka
uwezo
na msaada.
Atayatimiza
yote
aliyoyaanza.
4.
Ukamwachie kutenda
atakalo
kwako!
Kwa
hiyo ulale raha
na
kufurahiwa.
Comments
Post a Comment